Trending News>>

Griezmann amsikitikia Pogba kupitia kipindi kigumu Man Utd



Paris, Ufaransa. Mshambuliaji wa Ufaransa, Antoine Griezmann ameeleza kusikitishwa na kiungo wao, Paul Pogba akisema anahitaji kusaidiwa, kupendwa zaidi kipindi hiki anachokabiliwa na wakati mgumu.

Kauli hiyo ya Griezmann ameitoa baada ya Ufaransa kuilaza Bulgaria kwa mabao 4-1 kwenye mchezo wa kufuzu kwa Kombe la Dunia ambako Pogba alicheza vizuri, ingawa si kwa kiwango chake cha kawaida.

Alieleza kuwa Pogba anahitaji kuonyeshwa mapenzi ili aweze kurejesha kiwango cha ubora ambacho kimeporomoka kwa kiasi kikubwa.

Kikosi cha Ufaransa, Les Bleus kilirejea uwanjani hapo, Stade de France kwa mara ya kwanza tangu kidunguliwe na Ureno kwa bao la dakika za nyongeza kwenye fainali za Ulaya, Euro 2016, usiku ambao Pogba alikumbwa na jinamizi la kupotea kwa kiwango chake.

Kijana huyo mwenye miaka 23 amekuwa na wakati mgumu tangu atue Manchester United kwa ada ya uhamisho ya karibu Pauni 100 milioni akitokea Juventus na kupewa jukumu kubwa kwenye klabu hiyo mpya, jambo ambalo Griezmann anasisitiza ndilo linalomtesa.

Akizungumza na gazeti la L’Equipe baada ya mchezo huo, Griezmann alisema: “Pogba anahitaji kupendwa zaidi arejeshe kiwango chake. “Anacheza mchezo tofauti na uliozoeleka akiwa Juve, sasa Manchester ni timu tofauti, pia kikosi cha Ufaransa ni tofauti kabisa kimfumo,” aliongeza.

Griezmann, mshindi wa kiatu cha dhahabu kwa mabao Euro 2016 na tuzo ya mchezaji bora aliifungia mojawapo ya mabao manne nchi yake, alitengeneza jingine kwa mwenzake wa Atletico Madrid, Kevin Gameiro aliyefunga mawili.

Gamiero aling’ara katika mchezo huo wa kwanza kwenye kikosi cha Ufaransa kwa miaka mitano ambako alifurahia kushirikiana na mwenzake, Griezmann. Pia, kocha Dideir Deschamps alikuwa mwenye furaha kutokana na ushirikiano huo.

Akizungumza na gazeti la L’Equipe baada ya mchezo huo, Griezmann alisema: “Pogba anahitaji kupendwa zaidi arejeshe kiwango chake. “Anacheza mchezo tofauti na uliozoeleka akiwa Juve, sasa Manchester ni timu tofauti, pia kikosi cha Ufaransa ni tofauti kabisa kimfumo.”

No comments:

Powered by Blogger.