Kuna vitu vingi ambavyo unaweza kutumia kwa manufaa yako ili kufanya
wanawake wakuone unavutia. Amini usiamini, hivi vitu si lazima uwe
tajiri wala uwe na urembo wowote. Mwanzo kati ya vitu hivyo vingi ni
rahisi kuvitumia kwa urahisi. Hii hapa ni orodha ya mambo ambayo
ukiyazingatia yatakufanya wewe uwe na mnato kwa mwanamke yeyote yule.
1. Uwezo wako wa nishati
Nishati inaweza kuwa na mkusanyiko wa vitu kadhaa, kama vile kuhisi kwa
vipepeo ndani ya tumbo, kusuka, wasiwasi ama vitu tofauti kabisa. Kwa
mtizamo wa moja kwa moja, nishati inahusiana na yote yale ambayo
yanamfanya mwanamke kujiskia raha wakati anapokuona ama kutaka kuutumia
muda wake mwingi akiwa na wewe. Nishati inacheza nafasi kubwa katika
mapenzi kama wataka kumtongoza mwanamke na ufaulu kwa urahisi. Ili
kupeana nishati zaidi kila wakati unapokuwa na mwanamke, hakikisha kile
kikuu unachohitaji kufanya ni kumchekesha, kumsapraiz, umguse kwa bahati
mbaya mara kwa mara, kuwa mwenye michezo nk. Zote hizo zitamfanya
kukufikiria wewe mara 24/7.
2. Mbinu utakayoitumia kumsifu
Kulingana na utafiti kutoka NBC unadai ya kwamba wanawake wengi
hawajiskii huru kupewa ama kupokea sifa kutoka kwa wanaume. Lakini
usikatwe na tamaa! Vile ambavyo utampongeza mwanamke inaweza kucheza
pakubwa kufaulu kumpata mwanamke unayempendae baada ya muda. Afterall
ukimsifu kitofauti tofauti anaweza kukubali ama kukuona kama wewe ni
mzaha kwake. So kuhepa aibu kama hizi ndogo ndogo, unafaa umsifu
mwanamke kwa jambo ambalo ni la kwake pekee, yaani kitu ambacho utamsifu
nacho hakipatikani kwa mwingine. Mfano waweza kumakinika kwa kitu
ambacho anafanya wakati flani na utumie ujuzi wako wa kiume kumsifia na
jambo hilo. Mfano unaweza kumsifu kwa uwezo wake wa kuimba, kuchora,
mtindo wake wa kutembea nk. [Soma: Mbinu ya kutongoza kwa wale
wanaojifunza]
3. Upambo wako
Si lazima uwe mwanamume wa kuvutia ili umvutie mwanamke. Utafiti
umebainisha kuwa wanawake hawavutiwi na urembo wa mwanamume, nywele zake
wala ngozi yake. Mwanzo kuwa mrembo kama mwanamume kuna ubaya wake
mwingi ikizingatiwa kuwa unaweza kuonekana kama pleya ambaye unapendwa
na wanawake wengi.
Kile ambacho unachohitajika hapa ni uhakikishe kuwa uwe nadhifu kimwili
na mavazi yako. Kufanya hivi kutakusaidia wewe kuonekana mtu timamu
halikadhalika inakufanya wewe kuwa na confidence ya kapproach demu
yeyote yule.
4. Ujuzi wako wa kutangamana
Lazima atleast uwe na ujuzi ambao utakusaidia wewe kuweza kutangamana na
wengine. Kama mwanamume lazima uwe na ujuzi ambao utakusaidia wewe
kutangamana na wengine kwa urahisi. Hii inamaanisha kuwa lazima uwe na
ujuzi flani wa kuongea na wanawake ndipo utakapojua jinsi ya kumfanya
apagawe na wewe.
5. Kiwango chako cha kujiamini
Kitu cha mwisho ambacho ni muhimu kwako kuwa nacho ni kujiamini.
Kujiamini ni njia moja wapo ya lazima uwe nayo ili uweze kuiteka hisia
ya mwanamke yeyote yule.[Soma: Njia za kuwa na confidence kama mwanaume]
KUMBUKA: Vitu vyote tulivyoeleza hapo juu havitakuwa na manufaa
yeyote yale iwapo kama hutaweza kujiamini kama mwanamume. Hivyo ni
lazima kwako kuhakikisha kuwa mwanzo unajijenga kwa kuwa na confidence.
Hii ni kuanzia kujitambua wewe mwenyewe bila kujishuku, kuongea bila
woga wowote wala kutoingiwa na wasiwasi wakati wowote ukiwa karibu na
mwanamke.
Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Apagawe Kwako
Reviewed by
Unknown
on
October 13, 2016
Rating:
5
No comments:
Post a Comment