UTAFITI uliofanywa na Chuo Kikuu cha State cha jijini New York nchini
Marekani unaeleza kuwa manii ni nzuri kwa wanawake kwani huwaondolea
msongo wa mawazo.
Pia, watafiti hao wamesema wanawake wanaofanya tendo la ndoa mara kwa
mara bila kutumia kinga (mapenzi salama) wanakuwa na kiwango kidogo cha
msongo wa mawazo na hufanya vizuri katika vipimo vya akili.
Hali hii wamesema wataalam hao kuwa inatokana na manii kuwa na kemikali
ambazo humfanya mtu kuwa vizuri kihisia, huongeza upendo/unyenyekevu,
huchochea mtu kupata usingizi na huwa na angalau aina tatu za kemikali
za kuondoa msongo wa mawazo (anti-depressants).
Utafiti huo uliofanywa kwa kuwahoji wanawake 293 kwa kufuatilia maisha
yao ya kujamiana dhidi ya afya za akili zao. Manii huwa na mchanganyiko
wa kemikali aina ya cortisol ambayo huongeza upendo, kemikali aina ya
esterone na oxytocin ambazo zote humfanya mtu kuwa vizuri kihisia.
Pia, huwa na homoni aina za ‘thyrotropin releasing hormone’, ambayo
huondoa msongo wa mawazo, melatonin ambayo huchochea usingizi na
serotonin ambayo ni homoni inayoondoa msongo wa mawazo.
Kutokana kuwapo kwa mchanganyiko wa kemikali na homoni hizo kwenye manii
Matokeo ya utafiti
Matokeo muhimu ya utafiti huu ambao umechapishwa katika jarida la
‘Archives of Sexual Behaviour’ ni kwamba hata baada ya baadhi ya
watafitiwa kuongeza kiwango chao cha kujamiana, wale ambao walikuwa
hawatumii kinga yoyote walikuwa na kiwango kidogo cha msongo wa mawazo
tofauti na wale ambao walikuwa wakitumia kinga kama kondomu wakati wa
kujamiana.
Pia, wanawake hawa ambao hawakutumia kinga walikuwa na kiwango kidogo
cha msongo wa mawazo tofauti na wale ambao hawakushiriki tendo la ndoa
kabisa.
Watafiti hao wamesema siyo tu kujamiana huongeza furaha kwa mwanamke na
hivyo kumwondolea msongo wa mawazo, bali kiwango cha furaha pia huendana
na wingi wa manii katika mili yao.
Hata hivyo, ushauri wa kitaalamu ni kuwa utafiti huu usiwe chanzo cha
watu kufanya mapenzi bila kinga bali uwe chanzo cha kufanya mapenzi
salama na mwenza unayemwamini.
Pia, tunakemea na kupinga wale wote wanaofanya vitendo vya usagaji kwani
ni hatari kwa afya zao kwani ni chanzo kimojawapo cha magonjwa ya
akili. Wiki ijayo tutakuletea mengi kuhusu uhusiano kati ya usagaji na
ugonjwa wa akili.
Je, Kujamiiana Huondoa Msongo wa Mawazo Kwa Wanawake?
Reviewed by
Unknown
on
October 13, 2016
Rating:
5
No comments:
Post a Comment