Utakubaliana na mimi kwamba wanaume wengi walioko kwenye ndoa wanakufa
mapema na kuwaacha wake zao, ingawa swali linabaki kuwa ni kwanini?
Zifuatazo ni sababu 6 za wanaume wengi walioko kwenye ndoa kufa mapema na kuwaacha wake zao.
1. Ugumu katika kufunguka.
Utakubaliana na mimi kwamba wanaume ni wagumu sana ten asana kufunguka
na kushirikisha mambo yao, wao wako tayari wafe na tai shingoni
wakijifanya hawaumii au hawasikii shida. Mkiwa na ishu kwenye ndo
mkaitwa sehemu muyaongee yeye kamwe hamumpati, anakwambia
mambo yetu tutasuluhisha wenyewe wakati ndani yanamla na kummaliza.
2. Ugumu katika kusamehe.
Kusamehe sio tu kwa faida ya anayesamehewa bali pia kwa afya yaw ewe
unayesamehe. Mzigo unaotokana na kusamehe hutuumiza sana mioyo yetu,
hata kama mara nyingine tunajifanya hatuna shida yeyote.
Unaposamehe unaachilia mzigo mkubwa, wanaume wao ni wagumu sana
kusamehe. Wako tayari wakubebe moyoni miaka, na tena watakukumbusha
uchungu wao kila wanapokuona. Hii inawala sana bila wao kujua.
3. Tabia hatarishi.
Wanaume wengi kwenye ndoa ndio wanaoongoza kushiriki tabia hatarishi
kama vile ulevi, anasa, ngono holela na hii huwaweka karibu zaidi na
jeneza kuliko wake zao
waliowaacha nyumbani wakiwadanganya kuwa wako mkutanoni mkoani.
4. Ugumu katika kujali afya.
Ni rahisi sana mwanaume akajisikia vibaya lakini asiende hospitalini
kuangalia afya, hata pale anapohimizwa kwenda bado anaweza kukwepa au
kubisha au hata kusema kuwa ameshakwenda au ameshakunywa dawa kumbe
mwongo.
Wako pia ambao wanaweza kupewa dawa na wasizitumie.
5. Msongo wa mawazo.
Wanaume ndio wabebaji wakubwa wa shehena za msongo wa mawazo “stress”
ingawa kwa nje wanajitahidi sana kuonyesha kuwa mambo yako shwari wakati
wanatafunwa ndani. Kaulize hospitalini, wanaokufa kwa presha ya kupanda
au ya kushuka, stroke, kusimama kwa
moyo, kupasuka kwa mishipa ya damu, matatizo ya mifupa, au kuumwa sana kichwa, halafu uliza ni jinsia gani.
Kuwa open, roho safi and less agressive.
Na Manyama.Com
Hizi Ndio Sababu Zinazowafanya Wanaume Kufa Mapema Kabla ya Wanawake
Reviewed by
Unknown
on
October 13, 2016
Rating:
5
No comments:
Post a Comment