Wamewakosea nini? Ni dhambi kuzaliwa mwanamke? Nani atawaepusha na kadhia hizi kama sio mimi na wewe? Imetosha!!!! Mimba na ndoa za utotoni zinaepukika chukua hatua kumlinda mtoto wa kike.
Ni kama mfungwa anayesubiria kunyongwa ama kuishi kwenye mateso makali
yasiyosimulika pale unapozaliwa wa kike katika mkoa wa Mara
ama Shinyanga, mikoa hii ndio vinara wa ndoa za utotoni na huku
kukisheheni vitendo vya kikatili vya ukeketeji.
Leo ni maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa
Kike Duniani ambapo kitaifa inaadhimishwa mkoani Shinyanga,
huku serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa Watoto Magereth Mussai kutoka
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akipinga
vikali watoto kukoseshwa haki yao ya msingi ya kupata elimu kwa
kukatishwa masomo na kuozeshwa katika umri mdogo na kushindwa kufikia
ndoto zao.
Kasi ya ndoa na mimba za utotoni
inaongezeka kila uchwao huku vyombo vya habari kupitia kwa Chama cha
Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa) vikiwa mstari wa mbele
kuibua madhambi wanayotendewa watoto wa kike ili kukomesha na kutokomeza
kabisa ukatili dhidi wa watoto wa kike.
Ni dhahiri Mungu anawaona wale wote
wanaotekeleza ukatili huu dhidi ya watoto wa kike na siku ya mwisho kila
mmoja atatoa hesabu ya matendo yake; bado nguvu inahitajika katika
mapambano dhidi ya ndoa na mimba za utotoni sambamba na ukeketaji kwani
kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Idadi ya Watu (UNFPA), inakadiriwa katika kipindi cha miaka kumi ijayo
wasichana wapatao milioni moja wanatarajiwa kuwa wameolewa katika umri
wa chini ya miaka 18 duniani kote.
MNAOWAKATILI WATOTO WA KIKE MUNGU ANAWAONA!!
Reviewed by Unknown
on
October 13, 2016
Rating: 5
No comments:
Post a Comment