Imelda Mtema, Risasi
SUPA-STAA Wema Isaac Sepetu ‘Madam’, amefunguka kuwa anachukizwa na watu
wanaomtolea matusi muigizaji mwenzake, Aunt Ezekiel, baada ya
kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa ya mzazi mwenza wa Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
Akizungumza na Za Motomoto News, Wema alisema unatakiwa ufike wakati
watu waelewe na waongozwe kwa akili zao za kuzaliwa kwa sababu hakuna
kitu kibaya ambacho amekifanya Aunt, kwa kuwa staa mwenzake huyo kwa
sasa ni mmoja wa familia hiyo.
“Jamani
hebu naomba kwanza wamuache Aunt, hana kosa lolote, hata kama ningekuwa
mimi hapa nisingeweza kuacha kwenda kwa sababu tayari ni familia na
hawezi kumuacha mumewe aende peke yake maana vitu vingine ni vya
kujiongeza tu, nachukizwa sana na jinsi wanavyomrushia maneno ya
kashfa,” alisema Wema.
Wema Sepetu Awashushua Wanaomsema Aunt na Zari
Reviewed by
Unknown
on
October 13, 2016
Rating:
5
No comments:
Post a Comment