Wahislamu Nigeria wamjia juu Rapa Falz..
Rapa Falz kutoka Nigeria amejikuta pabaya baada ya kundi la Waislamu nchini humo la The Muslim Rights Concern (MURIC) kumtaka afute video ya wimbo wake mpya wa ‘This is Nigeria’.
<iframe width="330" height="186" src="https://www.youtube.com/embed/UW_xEqCWrm0" frameborder="0" allow="autoplay; encrypted-media" allowfullscreen></iframe>
Kundi hilo la kiislamu limemtaka rapa Falz afute video hiyo ndani ya siku saba na kuwaomba radhi Waislamu la sivyo litachukua hatua nyingine kali za kisheria kwa madai kuwa video hiyo inaudhalilisha uislamu.
Video hiyo ya ‘This is Nigeria’ inaonesha wasichana waliovalia vazi la Hijab wakicheza muziki kwa staili maarufu ya kucheza nchini Nigeria ya ‘shaku shaku’.
Video hiyo pia sio tu imewagusa Waislamu pia imewachana viongozi wakubwa wa dini ya kikristo wanaoutumia injili kujiingizia kipato nchini humo.
Pia mashairi ya wimbo huo yametaja maovu yanayotendeka kwenye mitaa ya miji mikubwa kama uporaji kwa kutumia silaha na pia amezungumzia matatizo ya rushwa nchini humo kama janga la taifa.
Video hiyo mpaka sasa ina siku 7 tangu itoke na tayari imetazamwa mara milioni 4 huku maoni ya watazamaji wengi kwenye mtandao wa YouTube wakionekana kuipokea kwa mtazamo chanya.
Hata hivyo, Idea ya video ya wimbo huo imefanana kabisa na video ya ‘This is America’ ya Rapper Childish Gambino.
No comments:
Post a Comment