Mwanajeshi mmoja wa Tanzania auawa na wengine watano hali mbaya..
Kwenye Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Ulinzi Tanzania imesema kwamba kati tukio hilo limetokea Juni 3, 2018 huko Afrika ya Kati, ambapo kikosi hiko chenye askari 90 kilishambuliwa na waasi wanaojulikana kwa jina la Sirir, na kusababisha kifo cha askari huyo mmoja, kujeruhi 18 huku watano kati yao wakiwa katika hali mbaya zaidi.
Majeruhi wa shambulio hilo wamepelekwa katika Hospitali ya Kanda ya Umoja wa Mataifa iliyopo Bangui kupatiwa matibabu, huku utaratibu wa kuurejesha mwili wa marehemu nyumbani Tanzania zikiwa zinaendelea.
No comments:
Post a Comment