Trending News>>

Sheik mkuu ataja tarehe ya sikukuu..

Comments Off on Sheikh Mkuu ataja tarehe ya sikukuuu ya Eid El-Fitri 2018

Ikiwa waislamu wote duniani wanaendelea mfungo wa kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramdhan na leo ikiwa ni chungu cha 28 Mheshimiwa Mufti na  Sheikh Mkuu wa Tanzania Abubakar Bin Zuber Ally Mbwana ametoa taarifa rasmi kuwa sikukuu za Eid El-Fitri zitasherekewa siku ya Ijumaa June 15, 2018 na kumalizika Jumamosi Juni 16, 2018.


Amesema siku hizo mwezi unatarajiwa kuandamana kama ilivyo desturi ya sikuu hii ambayo huadhimishwa mara baada ya mwezi kuandama ambapo ametangaza kuwa misa ya sikukuuu hii itaswaliwa ndani ya viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.

Hayo yamebainishwa mara baada ya kutokea mkanganyiko wa watu wanaosema sikukuu hiyo kuadhimishwa siku ya Jumamosi na Jumapili huku wengine wakidai kufanyika siku ya Ijumaa na Jumamosi, hivyo taarifa hii maalumu toka kwa kiongozi mkuu wa dini ya Waislamu inasaidia kuleta majibu kamili juu ya sherehe hizi zinazoadhimishwa kila mwaka kulingana na mwandamo wa mwezi.

Aidha kuelekea kusherekea siku hii maeneo ya masoko yakiwemo Kariakoo yamefurika na watu mbalimbali kwa ajili ya kufanya manunuzi ya chakula na mavazi kwa ajili ya kusherekea sikukuu ya Eid El-Fitri.

Baraza linawatakia sikukuu njema ya Eid El-Fitri na kuwatakia amani tele katika kusherekea siku hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.