Trending News>>

Hivi ndivyo chakula chako kinaweza kugeuka na kuwa sumu

Hivi karibuni watafiti wa kutoka Chuo Kikuu cha Mauritius wamegundua na kutahadharisha kuwa vitambaa ambavyo hutumika jikoni huweza kusababisha sumu kwenye chakula. Sababu inayoweza kuchangia chakula chako kutokuwa na umuhimu katika mwili wako na hatimaye kusababisha madhara ni kwamba matumizi mbalimbali ya vitambaa hivyo kwa wakati mmoja hutoa mwanya kwa bakteria wajulikanao kama E.Coli kuingia ambao ndio hutengeneza sumu. Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la BBC, utafiti huo ulifanywa kwa vitambaa vya jikoni 100 ambavyo vilikuwa vimetumika kwa kipindi cha mwezi mmoja na iligundulika kwamba, asilimia 49 ya vitambaa hivyo vilikuwa na bakteria. Utafiti huu pia umebainisha kuwa matumizi ya vitambaa hivyo, au sponji na gloves za jikoni zikiwa mbichi ni hatari kwa afya na hivyo ni vyema vitumike vikiwa vikavu. Bakteria hawa wanaelezwa kuongezeka kutokana na ukubwa wa familia husika, uwepo wa watoto na wazee pamoja na wingi wa matumizi ya vitambaa hivyo. Moja wa watafiti wa utafiti huo, Dr Susheela Biranjia-Hurdoyal wa chuo hicho, ameeleza kuwa usafi katika kuandaa vyakula ambavyo sio mboga za majani uzingatiwe ili kuepuka matatizo ya kiafya. Utafiti huu umetolewa katika Mkutano wa Mwaka wa Jumuiya ya Maicrobaiolojia, Atlanta, Georgia nchini Marekani.


No comments:

Powered by Blogger.