Mzamiru Yassin ahamua Kiume
HABARI ndio hiyo mjue. Kiungo fundi wa Simba, Mzamiru Yassin, ameamua kiume na sasa anahesabu saa tu kabla ya kumwaga wino kuendelea kukipiga Msimbazi.
Mzamiru aliyekuwa akitajwa kutaka kuondoka klabuni hapo wakati mkataba wake ukiwa umeisha, ishu yake imefikia patamu na wakati wowote atasaini mkataba mpya ili aendelee kuitumikia timu yake iliyomtoa Manungu, Turiani alikokuwa akiichezea Mtibwa Sugar.
Akizungumza na Mwanaspoti, Mzamiru alisema ana asilimia 90 za kubaki Msimbazi kwa maelezo kila kitu kinaenda na kwamba ni vipengele vichache vinavyoendelea kujadiliwa ili ajue anasaini muda gani.
“Kwa mazungumzo tulipofikia sijaona kikwazo cha kuachana na Simba, kuna mambo machache ambayo tunayaweka sawa ndipo nitaamua nisaini mkataba wa muda gani,” alisema.
Pia alizungumzia kwa nini amebaki jijini Dar es Salaam, wakati timu ipo Kenya kwa ajili ya kucheza michuano ya Sportpesa.
“Nilikuwa naumwa, lakini naamini kesho (leo Jumamosi) ninaweza kwenda kujiunga na timu,” alisema na kuongeza huenda akaenda akiwa ameshasaini kabisa.
No comments:
Post a Comment