Flyover tazara kuzinduliwa Septemba
Dar es Salaam. Waziri wa Uchukuzi, Makame Mbarawa amesema barabara ya juu ya Tazara, itazinduliwa Septemba mwaka huu baada ya ujenzi kukamilika.
Profesa Mbarawa ameandika hayo katika ukurasa wake wa twitter, Juni 6 na kusema kuwa ujenzi huo kwa sasa unaelekea mwishoni.
“Ujenzi unaelekea mwishoni, tunaishuru Serikali ya Japan na mkandarasi kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction Co. Ltd,” amesema
Mkataba wa ujenzi kati ya Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) na Kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction Co. Ltd ulisainiwa Oktoba 15, mwaka 2015 na kushuhudiwa na Rais John Magufuli wakati huo akiwa Waziri wa Ujenzi.
Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo la Kimataifa (JICA), ina historia ya zaidi ya miaka thelathini katika kusaidia uboreshaji wa miundombinu ya usafirishaji jijini Dar es Salaam, ikiwemo ujenzi wa Daraja la Selander mnamo mwaka 1980.
No comments:
Post a Comment