Trending News>>

YONDANI, HAJI MANARA, & MBEYA CITY, WASHUSHIWA RUNGU NA BODI YA LIGI.

Kamati ya Bodi ya Ligi Kuu Bara (VPL), SIKU YA LEO Mei 3, 2018, imetangaza adhabu ilizotoa dhidi ya makosa yasio ya kiungwana yaliyojitokeza katika michezo mbalimbali ya ligi hiyo.
Kamati hiyo imetangaza kumfungia beki wa Yanga  Kelvin Yondani kutokucheza mchezo wowote wa ligi mpaka bodi itakopokaa tena kwa kosa la kumtemea mate mlinzi wa simba Asante Kwasi kwenye mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga ulichezwa jijini Dar es Salaam siku ya April 29 mwaka huu.
Beki Kelvin Yondani
Bodi hiyo pia imetoa onyo kali kwa msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara kufuatia kitendo chake cha kuingia uwanjani baada ya mchezo wa Simba na Yanga kuisha.
Msemaji wa Simba, Haji Manara
Kwa upande wao klabu ya Mbeya City imetozwa faini ya laki 5 kwa kosa la mashabiki wao kutupa mawe na chupa kwenye mchezo wao dhidi ya Yanga  uliochezwa katika dimba la sikoine jijini Mbeya.
Mashabiki wa Mbeya City
Adhabu hizi zote zimetangazwa na Boniface Wambura ambaye ni  Mtendaji wa Bodi ya Ligi.

No comments:

Powered by Blogger.