MAMBO YATAKAYOKUFANYA UDUMU KWENYE PENZI JIPYA
HAKUNA muda ambao hisia za mapenzi na msisimko huwa mkubwa kama kipindi ambacho upo kwenye penzi jipya. Ukiwauliza watu wengi leo ambao wanateswa na mapenzi, wanataÂmani siku zirudi nyuma ili warudie kufaidi mapenzi kama ilivyokuwa siku za mwanzomwanzo.
Hata hivyo, ni wachache wanaojua nini cha kufanya unapoanzisha penzi jipya ili hisia na msisimko unaoupata, udumu kwa muda mrefu na uendelee kuyafurahia maisha ya kimapenzi. Mapenzi ni kama nyumba, ukijenga msingi imara, nyumba yako itakuwa imara na ukijenga msingi legelege, usitegemee nyumba yako kuja kudumu baadaye.
Kama upo kwenye mapenzi mapya na unatamani raha na msisimko unaoupata leo udumu, ni vizuri ukazingatia mambo yafuatayo:
- MUONYESHE HESHIMA NA SHUKRANI
Wanandoa, wachumba au wapenzi wengi, hulalamika kwamba wenzi wao hawawaheshimu, hawana shukrani na ndiyo maana hawafurahii maisha yao ya kimapenzi. Unapokuwa kwenye hatua za mwanzo za mapenzi, jenga heshima kwa mwenzi wako bila kujali umri, cheo au hali ya kiuchumi. Hata kama mwenzi wako ana udhaifu fulani, kwa sababu umemÂpenda na kuamua kuwa naye, jifunze kumheshimu.
Pia jifunze kuwa na shukrani hata kwa yale mambo maÂdogo anayokufanyia. WenÂgi huwa hawaoni umuhimu wa kuwashukuru wenzi wao na matokeo yake wanajenga ufa amÂbao baadaye unasaÂbabisha matatizo makubwa.
Hata kama mwenzi wako ame k u n u n u l i a pipi, akikupa shukrani kwa sababu amekuÂfikiria ndiyo maana akakununulia. Hata kama mwenzi wako amekupa zawadi au kitu ambacho hujakipenda, badala ya kukimbilia kuÂkosoa, onyesha kwanza shukrani, kesho na kesÂhokutwa atapata nguvu ya kukutafutia vitu vizuri zaidi.
- PATA MUDA WA KUMCHUNÂGUZA KWA KINA
K u c Âh u n g u Âzana ninaÂkomaani Âsha hapa, siyo kuÂtaka kuÂjua kabla y a k o
alikuwa na nani au amewahi kutoka na nani, wahenga wanasema bata ukimcÂhunguza sana huwezi kumla. KuchunguÂzana ninakokuzungumzia hapa, ni vizuri kufuatilia kwa kina ili ujue mwenzi wako anapenda nini, hapendi nini, kitu gani kinamfurahisha na kitu gani kinamtia hasira.
Mchunguze akiwa na hasira anakuwaÂje na akiwa na furaha anakuwaje, anaÂpenda sana kufanya mambo gani (hobi) au anapenda sana zawadi za namna gani. Ukishamjua, ni rahisi sana kuishi naye hata pale anapokasirika au anaÂpokerwa na jambo fulani kwani tayari utakuwa unajua kwamba akiwa hivi, ujue amekasirika au akifanya hivi ujue jambo fulani halipendi.
Pia itakusaidia kwenda naye sawa kwa sababu akikasirika, utajua ufanye nini ili afurahi kwa sababu tayari unaviÂjua vitu vinavyomfurahisha. Ni makosa makubwa kufanya jambo wakati unajua kabisa mwenzi wako hapendi.
- JENGA UTARATIBU WA KUMUOMÂBA MSAMAHA UNAPOKOSEA
Wanaume wengi wanaamini kwamba hata wakikosea, hawatakiwi kuomba msamaha kwa sababu kuomba msamaÂha ni ishara ya udhaifu, matokeo yake wanaendekeza mfumo dume bila kujua kwamba mapenzi ni demokrasia!
Bila kujali kwamba wewe ni mwaÂnaume au mwanamke, mkubwa au mdogo, una fedha au huna, inapotokea umeziumiza hisia za mwenzi wako, iwe kwa jambo dogo au kubwa, ni lazima uombe msamaha na kuahidi kutorudia makosa.
Ukishajenga utaraÂtibu huu, hata kama mwenzi wako hakuwa na kawaida ya kuomÂba msamaha, taraÂtibu utambadilisha. Utashangaa na yeye anaomba msamaha na huo unakuwa mfuÂmo wa maisha yenu. Kuwa makini kwamba ukiomba msamaha leo, siyo kesho unarudia tena kosa lilelile, ataona unamÂfanyia makusudi.
Ukizingatia mambo haya machache, ukazidisha mapenzi na kumjali mwenÂzi wako, ukawa mwaÂminifu na mkweli, hisia tamu za mapenzi unazozihisi leo, zitadumu na u t a y a f u r a Âhia maisha yako ya kiÂmapenzi.
No comments:
Post a Comment