WAZIRI MKUU KUZAA BAADA YA KUINGIA OFISINI
WAZIRI Mkuu wa New Zealand, Jacinda Ardern anategemea kujifungua mwezi Juni mwaka huu na kumfanya kuwa kiongozi wa kwanza duniani tangu 1990 kujifungua akiwa ofisini, jambo ambalo watu wengine wanadai ni tatizo.
Tukio hilo hili halimhusu aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza, Tony Blair, ambaye alipata mtoto aitwaye Leo, kutoka kwa mkewe Cherie, jambo ambalo lilimfanya Blair ajikute ‘akimnyonyesha’ mtoto wake huyo kwa njia fulani huku akiwa anaendelea na kazi zake.
“Mwaka huu tutaungana na wazazi wengi wanaovaa kofia mbili. Nitakuwa waziri mkuu na mama, ambapo Clarke (Gayford) atakuwa Mwanamume wa Kwanza (mume wa waziri mkuu),” alitangaza Ardern mwenye umri wa miaka 37, akimtaja mwanamume huyo, mtangazaji katika kituo kimoja cha televisheni, kuwa ndiye mwenza wake katika ujauzito huo.
Clarke, ambaye pia ni mpenzi wa kuvua samaki, watashirikiana na Ardern kulea mtoto huyo wanayemtegemea.
Ardern atajifungua muda si mrefu tangu kushika wadhifa huo Oktoba 26, 2017 baada ya kushinda uchaguzi mkuu. Hata hivyo, mama huyo ambaye bado ni kijana anabidi kukabiliana na changamoto kadhaa kutoka kwa wapiga kura wake ambao wanaona ataongeza jukumu jingine la kuwa mama-mtoto hivi karibuni.
Pamoja na yote hayo, bado anafurahi kwamba atapata mtoto na kupitia njia ambayo wanawake wengine huipitia, yaani kuzaa. Hata hivyo, anasema anatekeleza majukumu yake kikamilifu ofisini na nyumbani ambapo ni lazima watu wafahamu pia kwamba yeye ni mwanamke.
No comments:
Post a Comment