Trending News>>

DEAL DONE, SANCHEZ MALI YA MAN UNITED, MKHITARYAN MALI YA ARSENAL


Alexis Sanchez.
Alexis Sanchez anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya muda wowote kuanzia sasa ndani ya Jiji la Manchester ili kukamilisha dili lake la kujiunga na Manchester United.

Vipimo hivyo vitafanyika kwenye viwanja vya mazoezi ya Carrington ili kukamilisha uhamisho wa mchezaji huyo akitokea Arsenal.

Wakati huohuo, winga wa United, Henrikh Mkhitaryan naye ameonekana mitaa ya London ikielezwa kuwa anaenda kukamilisha dili la kuhamia Arsenal kwa kubadilishana na Sanchez.

Arsenal inamshusha Mkhitaryan wakati ambapo pia inamuwania straika wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang kwa ada ya pauni milioni 44 licha ya kuwa Dortmund umegoma kumuuza.

Mkhitaryan alikuwa akiongozana na wakala wake, Mino Raiola ambaye ndiye anayesimamia dili hilo, hivyo muda wowote kuanzai sasa kila kitu kitakamilika na kitatangazwa.

No comments:

Powered by Blogger.