Trending News>>

UJAUZITO WA KIGOGO WADAIWA KUMFICHA MASOGANGE


UBUYU haujawahi kumuacha mtu salama hata siku moja kutokana na pilipili inayowekwa ndani yake kuwasha vilivyo! Muuza nyago mwenye umbo matata kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva, Agness Gerald ‘Masogange’, anadaiwa kuishi kwa kujifichaficha, eti kisa ni mjamzito.

UBUYU BIN’ UBUYU
Kwa mujibu wa mmwaga ubuyu, miezi kadhaa iliyopita, Masogange alinasa ujauzito wa kigogo mzito serekalini.
Ilidaiwa kuwa, kigogo huyo ndiye aliyemwekea Masogange sharti hilo zito la kutoonekanaonekana ovyo na ndiyo maana siku hizi mrembo huyo haonekani kwenye viwanja kama alivyozoeleka zamani kabla ya kuwa kitumbo ndii, badala yake amekuwa mtu wa kujifungia nyumbani kwake, Makongo jijini Dar!

MASOGANGE AADIMIKA VIWANJA
“Kwa sasa huwezi kumkuta Masogange kwenye kumbi za starehe kama zamani. Yeye ni kushinda ndani tu, hata marafiki zake wanamshangaa.
“Unaambiwa sasa hivi akitoka ni kwenda hospitalini tu kwa ajili ya kliniki na hata akienda huwa anajifunika ‘ninja’ usoni ili watu wasiomjue,” alidai mtoa ubuyu huyo kwa sharti la kutotajwa gazetini.

 AZAWADIWA NDINGA KALI
Chanzo hicho kiliendelea kumwaga ubuyu kuwa, kutokana na kunasa ujauzito huo, Masogange alizawadia ndinga kali na kigogo huyo kama zawadi ya kumbebea mimba kwani huko nyuma Masogange hakuwa na habari kabisa na gari kama walivyo warembo wengine.

IJUMAA WIKIENDA Vs MASOGANGE
Baada ya kunyapianyapia ubuyu huo na kuona mambo ni moto kwa upande wa bidada huyo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta na kumbana ili kupata ukweli juu ya ujauzito wake huo ambapo mambo yalikuwa ni hiviii…
Ijumaa Wikienda: Mambo
 vipi Masogange? Mbona umeadimika viwanjani, tatizo ni nini?
Masogange: Mambo poa tu, kuhusu kuadimika, siku hizi nimeamua tu kutulia nyumbani na ni kweli siyo rahisi kunionaona kama zamani.

Ijumaa Wikienda: Ni kwa nini umeamua hivyo au kuna kitu nyumna ya pazia?
Masogange: Nimeamua tu kubadilika kutoka maisha haya kwenda mengine.
Ijumaa Wikienda: Mbona inasemekana ni kwa sababu ya ujauzito ulionao wa kigogo mzito serikalini?
Masogange: (kicheko)… hapana. Kwa nini sasa nijifiche? Kama ipo, ipo tu na ninavyojua mtu huwezi kuficha jambo kama hilo.
Ijumaa Wikienda: Inawezekana unataka uonekane na mtoto au mwenye ‘mzigo’ hataki uonekane ovyo?
Masogange: Hakuna kitu kama hicho. Kama mimba ni ya kigogo ndiyo niifiche? Naomba nikupigie baadaye maana hapa nina kazi kidogo.
Ijumaa Wikienda: Okey.
Hata hivyo, Masogange hakupiga simu kama alivyahidi na hata alipopigiwa simu yake iliita bila kupokelewa.
UBUYU: IMELDA MTEMA, DAR

No comments:

Powered by Blogger.