Trending News>>

MALAIKA AKIRI KUFELI KATIKA HILI

MWIMBAJI anayefanya vizuri kwenye muziki wa Bongo Fleva, Diana Exavery ‘Malaika’, amefunguka kuwa, udhaifu wake mkubwa kwenye maisha ni kusimama mbele za watu na kujielezea yeye ni nani.
Akipiga stori na Showbiz-Xtra, Malaika alisema, katika maisha amekuwa na udhaifu tofauti tofauti lakini mkubwa kuliko wote ni kutokuwa na ujasiri wa kuweza kusimama mbele za watu na kujieleza.
“Nimewahi kufeli kwenye interview nyingi kwa sababu ya kutakiwa kujielezea, kwa kweli huu ni udhaifu wangu mkubwa, hali hii ni tofauti na nikiwa jukwaani niki-paform, kuimba jukwaani mbele ya mashabiki ni tofauti na kujielezea,” alisema Malaika.
ALLY KATALAMBULA | AMANI

No comments:

Powered by Blogger.