Trending News>>

Tetesi za usajili barani Ulaya, Kane akaribia Madrid

Klabu ya soka ya Napoli wanaonekana kukubali kumruhusu mlinzi wao wa kushoto Faouzi Ghoulam kwend Manchester United, United wamekuwa wakitafuta beki wa kushoto na sasa wapo tayari kuwapa Napoli £53m.
Tetesi kutoka Anfield zinasema huenda mgogoro kati ya Liverpool na kiungo wao Phellipe Coutinho ukaibuka upya baada ya kiungo huyo kusema kwamba hayuko tayari kukipiga hapo na anataka kwenda Barcelona.
Kuna dalili za winga na beki wa kushoto wa zamani wa Tottenham Gareth Bale kurejea katika timu hiyo baada ya Real Madrid kuonesha nia ya kuwapa Tottenham £150m pamoja na Bale ili kumpata Harry Kane.
Klabu ya Southampton wanataka kutumia kiasi cha pesa walichokipata kutoka kwa Southampton ili kumnunua mshambuliaji wa klabu ya Arsenal Theo Walcott ambaye wamekuwa wakimuwinda kwa muda sasa.
Baada ya jaribio lao kushindwa katika dirisha kubwa la usajili, sasa kocha wa Chelsea Antonio Conte anataka kwa mara nyingine tena amepiga hodi katika klabu ya Everton ili kumnasa Ross Barkley.

No comments:

Powered by Blogger.