Trending News>>

Sholo Mwamba Asakwa Na Polisi Kwa Utapeli


Msanii wa muziki wa singeli nchini, Seif Mwinyijuma ‘Sholo Mwamba’.
MSANII wa muziki wa singeli nchini, Seif Mwinyijuma ‘Sholo Mwamba’ anasakwa na polisi kwa tuhuma za utapeli baada ya kutanguliziwa fedha ili afanye shoo kwenye mkesha wa mwaka mpya, kwenye ukumbi wa Dar Live, lakini akaingilia mitini na kusababisha tafrani kwa mashabiki.

Akizungumzia tukio hilo, Meneja wa Dar Live, Rajabu Mteta ‘KP Mjomba’ alithibitisha kumlipa nusu ya fedha, Sholo Mwamba ili afanye shoo lakini hakutokea na wala hakutoa taarifa yoyote huku simu yake na meneja wake, Waso Wisso zikiwa hazipatikani.

“Nilikubaliana na Sholo Mwamba afanye shoo kwenye mkesha wa mwaka mpya, mkataba wa fedha nusu aliyochukua upo, lakini hakutokea kufanya shoo, hali iliyozua tafrani kwa mashabiki na kuona waandaji ni matapeli.

“Mashabiki walipoona Sholo Mwamba hajafanya shoo na wala hayupo walizua tafrani iliyosababisha uharibifu wa baadhi ya mali. Kitendo alichokifanya Sholo si kizuri kwani matangazo yote yalionesha atakuwepo kama alipatwa na tatizo angewasiliana na mimi lakini alichokifanya ni utapeli,” alidai Kp Mjomba.
Tayari RB namba KJN/RB/12/2018 imetolewa kwa ajili ya kumkamata.
Stori: Mwandishi wetu, Uwazi

No comments:

Powered by Blogger.