Trending News>>

Mo Salah mwanasoka bora Afrika 2017

Wengi wakitarajia na ndivyo ikivyotokea kwa Mohamed Salah kutangazwa mchezaji bora wa Afrika katika tuzo za CAF zilizofanyika mjini Accra usiku wa Alhamisi, Salah anapewa tuzo hiyo kwa mafanikio ndani ya 2017.
Salah amekuwa na mwaka mzuri sana ndani ya 2017 akizisaidia timu zake ya Misri kwenda kombe la dunia huku akiwa wa pili kwa mabao EPL na mwaka 2017 alifunga jumla ya mabao 39 na assist 18.
Timu ya taifa ya Misri ambao ndio mabingwa wa soka barani Afrika walitangazwa kuwa timu bora Afrika huku mshambuliaji chipukizi ikienda kwa kinda raia wa Ivory Coast Patson Daka.
Wakati Misri wakipata tuzo ya timu bora, kocha wao Hector Cupper alitwaa tuzo ya kocha bora huku tuzo ya mwanasoka bora Afrika kwa upande wa wanawake ikienda kwa Mnigeria Asisat Oshoala.

No comments:

Powered by Blogger.