Marekani yanuia kukata misaada kwa Palestina
Rais wa Marekani Donald Trump ametishia
kukata msaada wa kifedha kwa serikali ya Palestina, kwa maelezo kwamba
Marekani inawalipa mamia ya mamilioni ya dola za kimarekani kwa mwaka na
hakuna chochote inachoambulia , hakuna cha shukrani ama heshima kutoka
kwa taifa hilo.
Katika utamaduni aliojijengea rais wa Marekani ,Donald Trump wa utumizi wa mtandao wa kijamii wa twitter kama sehemu yake ya kutolea matamko , rais amesema kwamba Wapalestina hawana mpango wowote wa kuwa na mazungumzo ya maridhiano na amani na Israel na kuhoji uhalali wa Marekani kuendelea kujitoa kwa kiasi hicho.
Mwezi uliopita rais wa Palestina Mahmoud Abbas alitoa tamko la taifa lake kutokuwa tayari kupokea mpango wowote wa amani kutoka Marekani, baada ya mji wa Washington kuitambua Yerusalemu kama mji mkuu wa Israeli.
No comments:
Post a Comment