Trending News>>

Jinsi Barca wanavyotumia kipindi cha pili kama machinjio


Msimu huu Barcelona wanaonekana kuwa katika kiwango cha hali ya juu sana, timu inaonekana kuimarika haswa kuanzia katika eneo lao la ulinzi hadi ushambuliaji.
Hadi sasa Barcelona wanaongoza ligi wakiwa na jumla ya alama  54 ikiwa ni alama 19 juu ya wapinzani wao wakubwa Real Madrid na dalili ziko wazi kwamba Barcelona wanaenda kubeba La Liga msimu huu.
Lakini Barcelona wanaonekana msimu huu kutumia sana kipindi cha pili kufanya wanachotaka kwa wapinzani wao na ushindi mwingi msimu wa 2017/2018 wameupata katika kipindi cha pili.
Hadi sasa Barcelona wameshafunga mabao 81 na katika mabao hayo 81 inaonesha 67.9% wameyapata katika kipindi cha pili huku mfano sahihi ikiwa mechi yao na Real Betis wakifunga mabao 5 nusu saa ya kipindi cha pili.
Dakika 15 zile baada ya halftime inaonesha huwa ndio wakati mgumu sana kwa wapinzani wa Barcelona na mabao 19 yamefungwa na Barcelona ndani ya dakika hizo 15 baada ya halftime.
Lioneil Messi ambaye ndio kinara wa mabao La Liga na pia kinara wa mabao katila klabu ya Barcelona lakini Messi katika mabao 25 aliyofunga msimu huu kuna mabao 18 ambayo yamepatikana kipindi cha pili.

No comments:

Powered by Blogger.