Z’bar Heroes yaivua ubingwa Uganda
Zanzibar Heroes wameivua ubingwa Uganda The Cranes baada ya
kuwafunga 2-1 kwenye mchezo wa nusu fainali ya pili ya kombe la Chalenji
2017 nchini Kenya huku Heroes ikifuzu kucheza fainali ya michuano hiyo.
Uganda ambao ni mabingwa mara 14 wa kombe hilo linaloshirikisha mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, wamejikuta wakishindwa kutetea ubingwa wao waliouchukua mwaka 2015 nchini Ethiopia na kuwacha Zanziba watinge fainali ambapo watakutana na Kenya ambao ni wenyeji wa mashindano hayo kwa mwaka huu.
Zanzibar walitangulia kupata goli dakika ya 22 kipindi cha kwanza goli likifungwa na Abdul-aziz Makame baada ya mabeki wa Uganda kujichanganya kuokoa mpira wa kona uliopigwa na Adeyum Ahmed. Uganda walisawazisha bao dakika ya 28 kupitia kwa Nsibambi Derrick.
Mohamed Issa ‘Banka’ aliifungia Zanzibar Heroes bao la ushindi kwa mkwaju wa penati baada ya Ibrahim Hamad Ahmada kuangushwa kwenye eneo la hatari na Nsumbuga Joseph.

- Zanzibar imeshinda mechi yake ya pili dhidi ya Uganda katika mechi 15 zilizopita, timu hizo zimetoka sare mara mmoja huku Uganda wakiwa wameshinda katika mechi 12.
- Uganda wamepoteza nafasi ya kutwaa taji la CECAFA Challenge Cup kwa mara ya 15, wameshabeba mara 14 (ikiwa ndio taifa lililotwaa kombe hilo mara nyingi zaidi) hivyo watacheza dhidi ya Burundi kuwania mshindi wa tatu wa mashindano ya mwaka huu.
- Zanzibar Heroes itacheza mechi ya fainali dhidi ya wenyeji Kenya siku ya Jumapili December 17, 2017.
- Endapo Zanzibar watafanikiwa kutwaa taji la CECAFA Challenge Cup 2017, itakuwa ni mara yao ya pili kufanya hivyo na kukata ukame wa kulikosa kombe hilo tangu walipochukua mwaka 1995
No comments:
Post a Comment