Trending News>>

Z’bar Heroes kazi-kazi nusu fainali Challenge Cup

Na Abubakar Khatib Kisandu, Machakos Kenya
Nusu fainali za Mashindano ya Cecafa Senior Challenge Cup zinatarajiwa kupigwa leo Alhamisi ya Disemba 14 kati ya wenyeji Kenya dhidi ya Burundi huku nusu fainali ya pili itasukumwa kesho Ijumaa ya Disemba 15 kati ya Zanzibar Heroes dhidi ya mabingwa watetezi Uganda.
Michezo yote hiyo itachezwa saa 9:00 za Alasiri kwenye uwanja wa Moi hapa Kisumu nchini Kenya ambapo timu zote nne tayari zimeshafika mjini Kisumu kusubiri michezo hiyo huku mchezo wa fainali na wakugombea nafasi ya tatu itapigwa katika uwanja wa Kenyatta mjini Machakos.
Kuelekea michezo hiyo ya nusu fainali shaffihdauda.co.tz imefanikiwa kuzungumza na Nicholas Musonye ambaye ni katibu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) amesema maandalizi yote yamekamilika kuelekea michezo hiyo huku akiipa tano Zanzibar.
“Nusu fainali zitachezwa leo na kesho, mpaka sasa matayarisho yote yanaendelea vizuri, Zanzibar nawapenda wanavyocheza na ningekuwa naruhusiwa kupenda timu basi ngependa Zanzibar,” alisema Musonye.
Uganda ‘The Cranes’ ndiyo mabingwa watetezi wa michuano hiyo baada ya kutwaa taji hilo mwaka 2015 nchini Ethiopia wakiwafunga Rwanda 1-0 kwenye fainali iliyopigwa mjini Addis Ababa.

No comments:

Powered by Blogger.