Trending News>>

WASANII:Ramsey Noah amlilia Kanumba !!!

Dar es Salaam. Nyota wa filamu wa  Nollywood nchini Nigeria, Ramsey Noah amemkumbuka msanii mwenzake Steven Kanumba akisema ndiye aliyejenga daraja la  ushirikiano kati yao.

Amesema Kanumba ndiye aliyewezesha ushirikiano kati ya Nollywood na Bongo Movie nchini Tanzania. Walicheza filamu mbili pamoja za Moses na Devil’s Kingdom.

"Nimemkumbuka Kanumba aliyekuwa wa kwanza kunileta Tanzania na kushirikiana katika filamu. Sitamsahau alikua mtu mzuri mwenye kupenda udadisi, kujifunza kuthubutu," amesema Ramsey leo Alhamisi Desemba 14,2017.

Ramsey yupo nchini ambako ameshiriki kongamano la kutambua fursa kwa vijana chini kwa mwaliko wa kampuni ya Sahara Tanzania.

Amesema atakwenda kuwasha mshumaa na kuweka maua kwenye kaburi la Kanumba Jumamosi Desemba 16,2017.

"Nawaomba Watanzania muungane nami katika kuweka mshumaa kwenye kaburi la Kanumba pamoja na maua," amesema.

Kanumba alifariki dunia Aprili 7,2012 baada ya kutokea mzozo nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam na rafiki yake Elizabert Michael maarufu Lulu.

Lulu ambaye pia ni msanii wa filamu kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka miwili jela baada ya Mahakama Kuu kumtia hatiani kwa kumuua bila kukusudia Kanumba.

Mwananchi:

No comments:

Powered by Blogger.