Trending News>>

Z’bar Heroes imeshindwa kuondoka na ndoo Kenya

Zanzibar Heroes imepoteza nafasi ya kushinda kwa mara ya pili kombe la Chalenji baada ya kufungwa na Kenya kwa mikwaju ya penati 3-2 kufuatia sare ya kufungana 2-2 kwenye mchezo wa fainali uliochezwa kwa dakika 120.
Dakika 90 za mchezo huo zilimalizika huku matokeo yakiwa 1-1, zikaongezwa dakika 30 ambapo kila timu ilifunga bao hivyo dakika 120 kumalizika kwa sare ya kufungana 2-2.
Mikwaju ya penati ikapigwa ili kuamua Bingwa wa kombe la Chalenji 2017 ndipo Kenya wakafanikiwa kuibuka mabingwa.

No comments:

Powered by Blogger.