WENYE MSIMAMO
Wanawake daraja la kwanza wanaopendwa zaidi na wanaume ni wale wenye
msimamo, uelewa mkubwa wa mambo na maamuzi sahihi, wako makini kwenye
matendo yao na siku zote hufanya vitu kwa ajili ya kupata mafanikio.
WAPENDA USAWA
Aina ya pili inayohitajika katika katika ulimwengu wa kimapenzi ni
wanawake wanaoheshimu usawa wa jinsia, walio tayari kubeba majukumu ya
kifamilia kwa ulinganifu sawa na wanaume, wenye uwezo wa kuongoza jamii
kwa asilimia 50 kwa 50.
WANAOJUA MAPENZI
Wanawake wajuzi wa mambo ya faragha wanapendwa sana. Sifa yao kubwa ni
uwezo wa kutosheleza katika tendo la ndoa. Tafiti zinaonyesha kuwa
wanaume hupenda sana wanawake watundu katika mchezo wa sita kwa sita.
Mara nyingi wanatajwa kuwa na uwezo wa kuteka akili za wanaume bila
kujali sifa zao za nje au za ndani.
MARAFIKI
Wanawake wenye sifa sawa na rafiki ni aina ya nne inayowavutia wanaume.
Wao hutegemea zaidi nguvu ya kushawishi inayotokana na namna wanavyojali
na kujitolea kuhakikisha wanakuwa marafiki wa kweli kwenye shida na
raha kwa wapenzi wao. Si wakorofi, waungwana na wapenda amani. WA WAZI
Aina nyingine ya wanawake inayowavutia wanaume ni wenye msimamo na
uwazi. Si wepesi wa kuburuzwa katika maamuzi ya msingi kwa kisingizio
cha wao ni wanawake. Utafiti unaonesha wanawake wa aina hii wamekuwa
muhimu hasa kwa wanaume wenye tabia za ubabe na udhaifu katika uelewa wa
mambo.
WANAOJITEGEMEA
Wanawake wanaojitegemea wana soko kubwa kwa wanaume tofauti na akina
naomba vocha kila siku. Uchunguzi unaonyesha kuwa wanaume wa leo
hawapendi wanawake tegemezi, wasiokuwa na kazi na wanaoendekeza starehe
za upande mmoja. WASIO NA PRESHA
Nikisema wanawake wasiokuwa na presha namaanisha wasiolazimisha vitu
vitokee haraka haraka. Wao siku zote huacha mambo yatokee yenyewe na
kazi yao kuwa ni kutenda sehemu ya majukumu yao kama wapenzi.
MARIDADI
Kundi lingine la wanawake wanaopendwa na wanaume ni wanaozingatia usafi
na kujiremba. Wanaokwenda na wakati katika mavazi na mvuto wa nje.
Lakini pia ni welewa wa mazingira, si wasamba. Wanapendeza kwa
muonekano. WANAORIDHIKA
Wanawake ambao hulidhika na hali walizonazo ni kivutio kikubwa kwa
wanaume, hili ni kundi linalohitajika sana katika ulimwengu wa mapenzi
kwa upande wa wanaume ambao maisha ya sasa yamekuwa yakiwageuza kutoka
juu kwenda chini au chini juu. Kukubali hali zote bila kubadili tabia ni
sifa njema ya mwanamke. WA MMOJA
Wanawake wanaochagua mara moja na kutosheka na kuwa tayari kukwepa kila
aina ya vishawishi toka kwa wanaume ambao kimtazamo wana vitu vya ziada
zaidi ya waliowachagua mwanzo wanahitajika sana. “Niliye naye
ananitosheleza kwa kila kitu sitaki mtu mwingine.” Kundi la wanawake wa
aina hii ni adimu na muhimu sana.
Aina 10 ya wanawake wanaopendwa na wanaume
Reviewed by Unknown
on
December 18, 2017
Rating: 5
No comments:
Post a Comment