Trending News>>

Yaliyojiri Kwenye Mkutano Mkuu wa CCM Taifa – Dodoma


Hotuba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasilisha hoja ya utekelezaji wa ilani ya CCM ndani ya mkutano mkuu wa chama hicho mjini Dodoma leo.
“Serikali imeanzisha mfumo mpya ya ununuzi wa mbolea ambapo sasa mfuko wa mbolea umekuwa ukiuzwa kuanzia 50000 ahdi 60000. Serikali inahahikisha uchumi wa nchi yetu unakua kwa kuifanya kuwa nchi ya viwanda.

“Tunaimarisha usafiri jijini Dar es salaam kwa kuboresha mabasi yaendayo kasi. Kutokana na juhudi za serikali kuboresha miundombinu hasa katika barabara na njia nyingine za usafiri, sasa idadi ya watalii imeongezaka na kufikia milioni mbili.
“Serikali imeweka juhudi za kujenga maabara katika shule za sekondari 2141 kati ya 3614 nchini. Seriakali imweka jitihada za kuhakikisha wananchi wanapata maji safi kwa kwa urahisi,” Alisema Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. 

Balozi Seif Ali Idd
“Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imenunua meli mpya ya abiria na mizigo inayoendeleakutoa huduma. Serikali ya Zanzibar pia iko mbioni kununua meli mbili, moja kwaajili ya abiria na nyingine ya mafuta.

“Serikali imeendelea kuimarisha sekta ya afya kwa kufanya matengenezo na kupandisha hadhi hospitali mbalimbali nchini. Serikali ya Zanzibar imejenga bohari dawa ya kisasa ambayo ni mfano katika bara la Afrika. Katika utoaji wa huduma ya maji safi na salama imefikia asilimia 75 kwa mjini na asilimia 70 kwa vijijini,” alisema Balozi Idd.

VIDEO: FUATILIA HOTUBA HIZO HAPA

No comments:

Powered by Blogger.