Airtel Yatangaza GB Zaidi Bando za Yatosha Intaneti
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imekutana na watangazi wa radio
mbalimbali nchini na kuongelea ongezeko la faida za mteja katika huduma
za intaneti zinazotolewa na Airtel kupitia kuzinduliwa kwa bando mpya
za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ zilizozinduliwa mwanzoni mwa wiki hii
kwa lengo lengo la kuwapatia wateja na watumiaji wote wa intaneti bando
nafuu zaidi.
Meneja
Masoko Airtel Tanzania Anethy Muga alieleza kuwa bando Mpya ya ‘SMATIKA
na Yatosha Intaneti’ zinatoa uhuru kwa wateja wote kujichagulia bando
la intaneti KABAMBE wakati wowote, na kusisitiza kuwa mteja wa Airtel
ataweza kunufaika na SMATIKA na Yatosha Intaneti kwa kujipatia bado za
gharama nafuu ya hadi shilingi 200 na kupata MB 40. Vilevile ofa kabambe
ya ‘SMATIKA Yatosha bando’ itamuwezesha mteja wa AirtelKUSMATIKA NA 1GB ya Yatosha Intaneti kwa siku tatu mfululizo kwa shilingi elfu mbili tu”
Kwa
upande wake Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema “Yatosha
mpya inakupa bado za siku, wik, mwezi gharama nafuu kuliko zote nchini,
kwa mfano bado ya 5,000 zamani ilikuwa na GB 1, kwa sasa Yatosha
Intaneti Mpya unapata GB 2 kwa siku 7, vile vile kwa shilingi 10,000
zamani ulikuwa unapata bando la GB 2.5 kwa siku 7 lakini sasa
tumeliongeza zaidi unapata GB 6 zakutumia wiki nzima. Alieleza Muga
“SMATIKA
na Yatosha Intaneti’ ni ishara ya Airtel kuanza vyema shamrashamra
kusherehekea sikukuu kwa kuwapatia uhakika wateja na watumiaji wa
huduma ya intaneti wa kutoishiwa bando kwa muda mfupi, Ukiwa na Airtel Yatosha Intaneti hainaga kuzima data tena!” Alisisitiza Mmbando.
No comments:
Post a Comment