Wanaopotosha Takwimu za Taifa Kwa Kisingizio Vyuma Vimekazaka Kufikishwa Mahakamani
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kusema kuwa watu ambao wanasema
vyuma vimekaza na wale ambao wamekuwa wakisambaza takwimu mbalimbali za
kupikwa kukamatwa na kuwekwa ndani na baadaye kupelekwa mahakamani.
Magufuli
amesema hayo leo alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika jengo la ofisi
ya Taifa ya Takwimu Dodoma na kuwataka wananchi kuwa makini na masuala
ya takwimu pia amewataka kuwapuuza watu ambao wanasema vyuma vimekaza
ili hala watu wa Takwimu wanasema vyuma vimefunguka.
"Ukikosea
kutoa takwimu umeichafua nchi, takwimu ni kitu kibaya sana ndiyo maana
kuna watu wamebobea kwenye takwimu hivyo wananchi tuwasikilize watu wa
takwimu asitokee mtu mwingine akatoa takwimu tofauti na zile walizonazo
watu wa takwimu.
"Mtu
anasema vyuma vimekaza wakati watu wa takwimu wanasema vyuma
vimefunguka watu hawa wanatakiwa kukamatwa na kuwekwa ndani ili
wakajifunze kutoa takwimu huko" alisema Rais Magufuli
Mbali
na hilo Rais Magufuli ameagiza watu ambao watatoa taarifa zozote ambazo
zipo kinyume na takwimu walizonazo watu wa takwimu wafikishwe
mahakamani ....."Mimi ningekuwa hakimu watu wa namna hiyo wangepewa
adhabu zote mbili kulipa faini na kufungwa"
“Ninawaomba Watanzania mpuuze uzushi unaoendelea kwenye mitandao ya kijamii kwamba uchumi umeshuka.
"wanaosema
vyuma vimebana, vitabana tu kwa wale waliokuwa wamezoea fedha za bure
bure, na vitaedelea kubana kweli kweli Lakini kwa wale wanaochapa kazi,
kwa mfano wakazi wa Lindi na Mtwara, walikuwa wanauza korosho saa
nyingine kwa bei ya chini mpaka elfu 2 kwa kilo, sasa elfu 4 kwa kilo.
"Wale
vyuma haviwezi vikabana, wale vyuma vimeachia, nasikia wanaamua hata
mbuzi kuzinywesha bia, kule vyuma vimefungua., hivyo wapuuzieni watu
wanaowadanganya vyuma vimekaza”, amesema Rais Magufuli.
Mbali
na hilo Magufuli amewataka wananchi na taasisi mbalimbali wakitaka
takwimu yoyote ile waende ofisi ya Takwimu na wasithubutu kutoa takwimu
ambazo zinapingana na zile zilizopo ofisi ya takwimu.
No comments:
Post a Comment