WAKIMBIZI WAIOMBA SERIKALI YA TANZANIA KUWAFUNGULIA SOKO LA BIDHAA ZAO
Mtaalamu
wa Masuala ya Ukatili wa Kijinsia na Ustawi wa Jamii kutoka Shirika la
Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Ofisi ndogo ya Kibondo akizungumza
na Wanawake wakimbizi wa Kambi ya Mtendeli iliyopo katika Wilaya ya
Kakonko Mkoani Kigoma juu ya Biashara ya ufumaji wa bidhaa kwa wanawake
hao waishio ndani ya kambi hiyo na kupatiwa ujuzi wa kuweza kujiongezea
kipato.
Muwezeshaji
wa Wanawake wa kutoka Shirika la IRC linalofadhiliwa na UNHCR,Beatrice
Emmanuel akitoa maelezo namna kikundi cha wanawake wafumaji wanavyoweza
kujiongezea kipato katika familia zao kwa kutengeneza na kuuza bidhaa
zao katika soko la pamoja linalojumuisha wakimbizi na Watanzania
wanaoishi katika vijiji vya jirani na eneo la kambi ya wakimbizi ya
Mtendeli. Pia wageni mbalimbali wanaowatembelea eneo la kambi kwa ajili
ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali ikiwemo wahisani na wadau
mbalimbali. lengo la mradi huu wa ufumaji ni kuwawezesha wanawake kupata
ujuzi utaowawezesha kujiongezea kipato ili pindi watakaporejea nchini
mwao kila mwanamke aweze kuwa na shughuli inayoweza kumuingizia kipato
Afisa
Uzalishaji kutoka IRC, Foibe Julius, akitoa maelekezo ya namna ya
kusuka vikapu kwa mmoja wa Mwanamke Mkimbizi anayeishi katika kambi ya
Wakimbizi ya Mtendeli iliyopo katika Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma
Msaidizi
Mkuu wa Makazi katika kambi ya Wakimbizi ya Mtendeli- Lulu Malima
akiangalia moja ya Bidhaa zilizofumwa na Wanawake wakimbizi wa kambi
hiyo ambao wameweza kuuza na kujiongezea kipato ili kuweza kujikimu
katika maisha yao.
Wanawake
wanaoishi katika kambi ya Wakaimbizi ya Mtendeli ya Wilaya ya Kakonko
mkoa wa Kigoma wakipanga bidhaa zao katika hali ya usafi ili kuwawezesha
wanunuzikuziona kwa urahisi katika eneo lao na kununua.
Mmoja
ya Wanawake kutoka kambi ya Wakimbizi ya Mtendeli Wilaya ya Kakonko
akifuma kikapu katika eneo la mafunzo linalofadhiliwa na UNHCR kupitia
shirika la IRCWanawakewaishio katika kambi ya Wakimbizi ya Mtendeli wakifuma vikapu katika eneo la mafunzo linalofadhiliwa na UNHCR kupitia shirika la IRC
Wanawake waishio katika kambi ya Wakimbizi ya Mtendeli Wilaya ya Kakonko Wakifuma Vikapu katika eneo la mafunzo linalofadhiliwa na UNHCR kupitia shirika la IRC
No comments:
Post a Comment