Ufafanuzi Kuhusu Lulu Kusamehewa na Rais Magufuli
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, Juma Malewa amesema katika msamaha
uliotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli siku ya uhuru Desemba 9, 2017 haukumuhusu msaani wa filamu
Elizabeth Michael maarufu kama Lulu.
Jenerali
Malewa amefafanua kuwa mchakato wa kuanza kuangalia wafungwa
wakupunguziwa vifungo na kusamehewa haukumuhusisha Elizabeth Michael
kutokana na yeye kuingia gerezani wakati tayari mchakato wa kuangalia
wafungwa wa kusamehewa na kupunguziwa vifungo ulikuwa umeshaisha
"Msamaha
huu haukumuhusu yeye kwa sababu aliingia magereza wakati tayari zoezi
hili lilikuwa limekamilika, kwahiyo labda misamaha ijayo kama itakuwepo
lakini katika hii haikumuhusu",amesema Kamishna Malewa.
Kamishna
Malewa pia ameeleza kuwa vipo vigezo vingi vinavyoweza kumfanya
mfungwa asamehewe ama kupunguziwa kifungo kutokana na kosa na muda wa
kifungo chake na kwamba misamaha inatofautiana kutokana na kosa kama
endapo mfungwa atafata taratibu na kuonekana amerekebishika anaweza
kupata msamaha na mengine mengi.
Desemba
9 mwaka huu siku ya uhuru kwa mujibu ya ibara ya 45 ya katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais John Pombe Magufuli alitoa msamaha
kwa wafungwa 61 waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa na wawili Nguza
Viking (Babu Seya ) na Johnson Nguza (Papii Kocha ) waliohukumiwa
kifungo cha maisha jela na wengine kupunguziwa vifungo vyao.
No comments:
Post a Comment