Trending News>>

Real Madrid imeifikia rekodi ya FC Barcelona leo!!!!



Club ya Real Madrid ya Hispania usiku wa December 16 2017 ilikuwa Dubai kucheza mchezo wake wa fainali ya Club Bingwa dunia dhidi ya club ya Gremio.

Real Madrid walishusha kikosi chao kamili kuwania taji hilo la club Bingwa Dunia, jambo ambalo liliwasaidia na kuwafanya waibuke na ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Staa wao Cristiano Ronaldo, hata hivyo Ronaldo anaweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa michuano hiyo kwa kufikisha goli la saba

Ushindi wa 1-0 umeifanya Real Madrid kutwaa taji lake la tatu la club Bingwa dunia sawa na wapinzani wao wa jadi FC Barcelona ambao nao wamefanikiwa kutwaa taji hilo mara tatu.

No comments:

Powered by Blogger.