Rais wa Zanzibar aahidi zawadi kwa Zanzibar Heroes, Wizara husika kushiriki kikamilifu katika fainali leo
Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein ametoa
salamu za pongezi kwa vijana wa timu ya taifa Zanzibar heroes kwa
hatua nzuri waliyoifikia kuingia fainali katika mashindano ya CECAFA
yanayoendelea nchini Kenya.
Akizungumza na Waandishi
wa habari kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Waziri wa Habari, Utalii,
Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma amesema kutokana na hatua
iliyofikia timu hiyo kwa jitihada waliyoiyonesha vijana hao katika
michuano hiyo Dk. Shein chini ya serikali yake ameahidi kuwapa zawadi
vijana wa Zanzibar heroes pindi watakapo rejea Zanzibar.
Amesema kutokana na
uwezo waliouonesha wachezaji wa timu hiyo serikali imeadhimia kutoa
tunzo maalum kwa vijana hao pamoja na kuwatengezea mazingira bora
katika uimarishaji wa timu hiyo pamoja na sekta ya michezo hapa
Zanzibar.
Hata hivyo Rashid
amesema endapo timu hiyo itarudi Zanzibar na kombe la ushindi kupitia
michuano hiyo Dk. Shein amesema atatoa zawadi mara mbili yake na
aliyoiahidi kwa vijana wa heroes.
Amesema serikali chini
ya Wizara yenye dhamana ya michezo itashiriki kikamilifu katika
fainali ili kuipa motisha timu hiyo huko nchini Kenya na wataandaliwa
mazingira mazuri ya usafiri watakapo maliza mashindano hayo ili
kurejea nyumbani Zanzibar.
Serikali imesema
itaziendeleza timu zake za taifa zote zikiwemo timu za mipira za
miguu,mipira ya mikono na mashindano mengine yote.
Amina Omar Zanzibar24
No comments:
Post a Comment