Polisi TAZARA Watoa Onyo kwa Wahalifu.
Kamanda
wa Polisi Kikosi cha TAZARA Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi
Patrick Byatao akimkabidhi cheti cha utendaji bora WP Nina Dachi wa
kikosi hicho baada ya kufanya vizuri katika kazi zake ambapo
alifanikisha kuzuia wizi wa mafuta katika reli ya TAZARA hivi karibuni.
Na. Jeshi la Polisi.
Jeshi la Polisi nchini limewaonya baadhi
ya watumishi wasio waaminifu wanaofanya kazi katika Reli ya Tanzania na
Zambia (TAZARA) ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya wizi wa
mafuta na miundombinu mbalimbali ya shirika hilo kuacha mara moja.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es
Salaam na Kamanda wa Polisi, Kikosi cha TAZARA Kamishna Msaidizi
Mwandamizi Patrick Byatao wakati wa hafla fupi ya kuwatunukia zawadi
baadhi ya Askari waliofanya vizuri katika kuhakikisha usalama wa
miundombinu ya shirika hilo ambapo baadhi yao walifanikiwa kuwakamata
watumishi wa shirika hilo wakiiba mafuta.
Amesema
katika siku za karibuni kumekuwa na matukio kadhaa ya watumishi wa
shirika hilo wasio waaminifu ambapo wamekuwa wakilitia hasara shirika
hilo jambo ambalo amesema wanaendelea kuimarisha usalama ili kuhakikisha
kuwa wanawadhibiti.
Kamanda
wa Polisi Kikosi cha TAZARA Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi
Patrick Byatao akimkabidhi cheti cha utendaji bora mmoja wa askari wa
kikosi hicho baada ya kufanya vizuri katika kazi zake ambapo
alifanikisha kuzuia wizi wa mafuta katika reli ya TAZARA hivi karibuni.
Kamanda
wa Polisi Kikosi cha TAZARA Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi
Patrick Byatao akimkabidhi zawadi ya jiko la gesi mmoja wa askari wa
kikosi hicho baada ya kufanya vizuri katika kazi zake ambapo
alifanikisha kuzuia wizi wa mafuta katika reli ya TAZARA hivi karibuni.
Kamanda
wa Polisi Kikosi cha TAZARA Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi
Patrick Byatao akikagua gwaride wakati wa hafla fupi ya kuwatunuku
askari waliofanya vizuri kwa mwaka 2017 katika kikosi hicho ambapo kwa
kiasi kikubwa wamezuia wizi wa mafuta katika reli ya TAZARA. (Picha na
Jeshi la Polisi)
Byatao amesema Kikosi hicho
kitaendelea kufanya operesheni za mara kwa mara ili kuhakikisha
wanakomesha tabia hiyo ambayo imekuwa ikidhoofisha utendaji wa TAZARA
pamoja na kuitia hasara Serikali.
Akizungumzia utoaji wa zawadi hizo.
Byatao amesema askari hao kumi wamefanya vizuri kwa kujituma katika
kipindi cha mwaka 2017 hivyo kwa mujibu wa taratibu za Jeshi la Polisi
ni vyema kuwazawadia ili kuongeza morali yao ya kazi na kuwafanya
wengine kuendelea kujituma zaidi.
Kwa upande wake mmoja wa Askari waliopata
zawadi baada ya kufanya vizuri WP Nina Dachi amewaasa askari wenzake
kuendelea kufanya kazi kwa umakini ili kuhakikisha kuwa miundominu ya
shirika hilo inakuwa salama wakati wote.
No comments:
Post a Comment