Mzunguko Wa Kwanza England… Mambo Yamekwisha
Kila timu imeonyesha kiwango chake, baadhi ya wachezaji wameonyesha ubora wao uwanjani huku wengine wakiwa ni wale ambao walikuwa hawatarajiwi kuwika na wengine wakiwa ni wale ambao walikuwa wanapewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri.
Tayari Manchester City wameongoz a kwenye mzunguko huu wakiwa hawajapoteza mchezo hata mmoja kati ya 18 ambayo wamecheza hadi sasa.
Wachambuzi wa masuala ya soka wameshawapa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa, makocha kadhaa wa Ligi Kuu England wameshawatangaza kama wapinzani sahihi wa ubingwa wa England msimu huu.
Kocha Pep Guardiola, ametengeneza kikosi imara sana ambacho kimeonekana kuweza kuteka kila timu kwenye ligi hiyo kwa sasa.
Tayari amefanikiwa kuibuka na ushindi dhidi ya timu zote kubwa kwenye Ligi Kuu England msimu huu, amewafunga Man United, Chelsea, Arsenal, Tottenham Hortspur pamoja na Liverpool ambazo zilikuwa zinapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa msimu huu.
Tayari kwenye michezo yao msimu huu imetoka sare michezo miwili tu ikiwa imeshinda 16 na huo mchezo mmoja haijatoka dhidi ya timu kubwa bali ilitoka sare dhidi ya Everton ambapo ilikuwa sare ya bao 1-1.
Hii inaonyesha kuwa City imejidhatiti kwa kiwango cha hali ya juu kwani mpaka sasa imedondosha pointi mbili tu.
Wakati wa o wakifanya hivyo timu inayoshika nafasi ya pili, Manchester United yenyewe imepoteza michezo mitatu ambayo ni sawa na pointi tisa na kutoka sare mara mbili ambazo ni sawa na pointi nne, jumla wenyewe wamepoteza pointi 10 kwenye michezo 18 ya mwanzoni mwa ligi
Hata hivyo, City wanaweza kupoteza, lakini siyo rahisi kwao kudondosha pointi kumi na mbili kwenye mzunguko wa pili wa ligi hali ambayo inaonyesha kuwa wanaweza kutangaza ubingwa wa England mapema zaidi mwakani.
Faida nyingine ambayo City wanayo ni kwamba wachezaj i wao wote m a h i r i wameend e l e a kuwa imara, hawajapata mt i k i s i k o m k u b w a kuanzia msimu umeanza.
Mastaa wa timu hiyo Kevin De Bruyne, Raheem Sterling na wengine wengi wamebaki kwenye ubora wao, hakuna hata m m o j a amb a y e ameweza k u p a t a majeraha a u kadi amb a y o imeweza kuwafanya wakakosa mchezo muhimu wa timu hiyo.
City wamekuwa na kikosi kilekile kwa kipindi chote cha msimu mzima, hii ni kama ilivyokuwa kwa Chelsea wakati wanachukua ubingwa msimu uliopita au nyuma yake wakati Leicester nao hawakuwa na majeruhi wala kadi nyekundu.
MANCHESTER INAWEZA KUMALIZA WA PILI
Timu nyingi ambazo zimekuwa zikiwania nafasi ya ubingwa wa Ligi Kuu England zimekuwa zikifanya vibaya sana kwenye mbio hizo.
United imekuwa ikiwategemea wachezaji wengi ambao mashabiki wao walikuwa hawawategemei kuwa wanaweza kufanya makubwa msimu huu.
Pamoja na Romelu Lukaku kufikisha mabao kumi kwenye L i g i K u u E n g l a n d lakini wamekuwa wakipata msaada mkubwa kutoka kwa Jesse Lingard ambaye ameamka na kufunga mabao manne kwenye michezo mitano na kuonyesha kuwa ni msaada mkubwa kwa kocha Jose Mourinho.
Huku pia timu hiyo ikipata huduma safi kutoka kwa kipa wao David de Gea ambaye amekuwa akiokoa michomo kadhaa ambayo ingewashinda makipa wengine.
Kukosa ubingwa kwa Jose Mourinho hakuwezi kuwa na faida hata kidogo hata kama atamaliza katika nafasi ya pili kwenye ligi hiyo kwa kuwa sasa itakuwa ni miaka mitano bila ubingwa wa England jambo ambalo mabosi hao hawawezi kuvumilia.
Hili linaonekana kuwa pigo kwa Manchester kwa kuwa hawajazoea maisha ya namna hii, hivyo kocha Jose Mourinho kuwafuta machozi basi angalau anatakiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya jambo ambalo pia linaonekana kuwa gumu kwake.
United ni lazima wapambane kama wanataka kumaliza kwenye nafasi ya pili kwa kuwa inawaniwa pia na Arsenal ambao wapo nyuma yao kwa pointi tisa, lakini kwa mwendo wa timu zote ni rahisi kuwafikia.
Lakini pia inawindwa na Liverpool pamoja na Chelsea ambazo zote zimekuwa kwenye mwendo wa kufanana hakuna hata moja ambayo ina uhakika.
Man United wamepoteza michezo mitatu kwenye mechi 18, Liverpool wamepoteza michezo miwili, Chelsea wamepoteza minne huku Arsenal wakipoteza michezo mitano.
Liverpool wenyewe wamekuwa wakipata msaada tosha toka kwa Mohamed Salah ambaye amekuwa akiwafungia kwenye kila mchezo muhimu.
Salah kwa sasa ndiye kinara kwenye ufungaji katika Ligi Kuu England akiwa amefunga mabao 14 na anatajwa kuwa usajili bora zaidi msimu huu.
Kwa ujumla mchezaji huyo amefanikiwa kufunga mabao 20 kwenye michuano yote akiwa ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa kwenye msimu wa kwanza na kufunga mabao 20 ndani ya kikosi cha Liverpool.
Ameweza kuwazidi mastaa wenye heshima kwenye timu hiyo kama Luis Suarez, Fernando Torres, Michael Owen na Robbie Fowler ambao hawakufika mabao 20 kwa msimu wao wa kwanza.
Kwa upande wa Chelsea wenyewe kwa sasa wapo nafasi ya tatu na kocha wa timu hiyo Antonio Conte, ameshasema kuwa hana presha tena kwa kuwa wameshamaliza mbio za ubingwa.
Kocha huyo amekuwa wa pili kukiri kuwa Manchester City ndiyo wanatakiwa kutwaa ubingwa huo msimu huu.
Timu hiyo kwa sasa ipo nyuma ya City kwa pointi 14, ambazo zinaonekana ni nyingi sana kuzipindua kwenye mzunguko wa pili wa ligi hiyo.
Kocha huyo amesema siyo kwamba wamefanya vibaya, bali Manchester City wameonyesha uwezo wa juu zaidi kuliko ilivyokuwa ikitegemewa mwanzoni mwa msimu huu.
No comments:
Post a Comment