Trending News>>

Msigwa awataka Chadema wachome nyumba yake akihama


Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa amewataka wananchi wa Iringa Mjini kuchoma magari na nyumba yake endapo atakihama Chama hicho na kuhamia CCM.

Mhe. Msigwa amesema hayo baada ya kupata simu nyingi za watu wakimrubuni kuhamia CCM na kusema kwamba kitendo hicho hakitawezekana katika maisha yake kwani atakuwa amepoteza heshima na dhamana aliyopatiwa na wananchi wa Manispaa ya Iringa .

“Nikihamia CCM wananchi wa Iringa wachome nyumba yangu  na magari yangu. Sikuingia bungeni kwa sababu nataka hela ila nimeingia kwa sababu kuna hoja, kuna agenda na kozi kama chama tunapigania. Mkome kabisa kunipigia simu, mimi sina bei itakayonihamisha CHADEMA,” amesema  Msigwa huku akifafanua jinsi watu hao walivyoanza kumrubuni kwa njia ya simu.

“Walianza kunipigia kwa kujifanya marafiki zangu na baadae wakaanza kunipanga na kunirubuni kwamba Mzee ananikubali na wala hana shida na mimi hivyo nikiingia CCM nitapata nafasi, nimewakemea na nimeonya wasinipie simu na sasa hivi wameacha ila naahidi wakinipia tena nitawarekodi niwaanike hadharani” I am not that ‘cheap’ wakatafute wengine.” amesema Msigwa.

Kauli hiyo ya Mhe. Msigwa inakuja ikiwa ni siku chache zimepita tangu aliyekuwa Mbunge wa jimbo Siha,  Dkt Godwin Aloyce Mollel (CHADEMA) kujiuzulu nafasi yake na kuhamia CCM.

No comments:

Powered by Blogger.