Mfumo wa usajili watengamaa Tanzania..
Jitihada za Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) za kuwasiliana na Mwendeshaji wa mfumo huo
waliokasimiwa na Shirikisho la soka la Kimataifa (FIFA) walioko Tunis,
Tunisia ili kuziwezesha timu kufanya usajili, zimefanikiwa.
Mtandao huo kwa sasa upo wazi. Hivyo
TFF inazitaka timu zote sasa kukamilisha usajili kuanzia pale
walipokwama. Timu zinatakiwa kusajili kabla ya Desemba 23, mwaka huu.
Desemba 15, mwaka huu mfumo wa usajili
kwa njia ya TMS ulifeli hali iliyosababisha vilabu kushindwa kukamilisha
usajili kwa wakati kupitia mfumo huo.
Katika mawasiliano na kampuni hiyo,
FIFA na CAF wamekuwa wakipewa Taarifa ya kila hatua inayochukuliwa na
TFF hadi mfumo huo kufunguka leo Desemba 19, 2017.
Bado TFF inasisitiza vilabu vyote kuzingatia kusajili kwa wakati pale inapotokea dirisha la usajili limefunguliwa.
No comments:
Post a Comment