Jifunze umuhimu wa CV bora (MAKALA)
Hakikisha inakuwa fupi na sahihi. CV kwaajili ya kuombea kazi haipaswi kuwa zaidi ya kurasa mbili, na yafaa ijumuishe stadi, ujuzi na uzoefu ambao unafaa zaidi kwa kazi unayoiomba.
Mwajiri atataka kupata taarifa zifuatazo kwenye CV yako:
Maelezo Binafsi
Weka jina lako na anwani, nambari ya simu, na barua pepe (email). Unaweza kuongeza utaifa wako, jinsia na tarehe ya kuzaliwa.
Profaili Binafsi
Hii ni hiari, lakini inaweza kuwa na
ufanisi sana katika kufupisha maeneo yako ya utaalamu na sifa. Ni vizuri
kujumuisha shauku yako juu ya kufanya kazi unayoiomba na nini
kinachokuchochea kwenye sekta hiyo. Tumia maneno muhimu na mafupi.
Ujuzi Muhimu
Jumuisha ujuzi wowote uliojifunza kama ujuzi wa kompyuta, uandishi, IT n.k.. Eleza pia nini unadhani ni ujuzi wako binafsi.
Historia ya Ajira
Anza na mwajiri wako wa sasa au wa
mwisho na uandike kwa mtililiko. Unapaswa kuingiza tarehe ya ajira, cheo
chako, jina la mwajiri, asili ya biashara, majukumu pamoja na
mafanikio.
Elimu na Sifa
Andika kwa mpangilio orodha fupi ya
sifa za shule, chuo au chuo kikuu, pamoja na daraja ulizopata. Kisha
orodhesha sifa yoyote zaidi uliyopata, pamoja na majina ya mamlaka
zilizotoa vyeti. Ikiwa unasoma kwa sasa, taja unachosomea pamoja na
matokeo yoyote yaliyopatikana hadi sasaChanzo: Umoja Media
No comments:
Post a Comment