Trending News>>

Liverpool vs Leicester, Leicester wanaweza kuwa matatizoni zaidi Anfield hii leo

Liverpool hawajawahi kupoteza mechi mbili mbele ya Leicester katika msimu mmoja tangu 1998/1999 na tayari wameshapoteza mechi moja ya EFL katikati ya mwezi wa 9 katika msimu huu wa 2017/18.
Hii inamaanisha Liverpool wanaweza kukubali kufungwa mara mbili na Leicester au wakaendeleza rekodi yako ya kutokukubali jambo hilo kwa Leicester ambao wamepoteza mechi 2 zilizopita kati ya 3 katika EPL.
Liverpool vs Leicester City ni kati ya michezo ambayo huwa inatoa idadi kubwa sana ya mabao kwani katika michezo 3 iliyopita baina ya timu hizi mbili ilishudiwa jumla ya mabao 14 yakifungwa katika michezo hiyo.
Jurgen Klopp anaonekana ndio kocha zaidi mbele ya Leicester tangu ajiunge na EPL, Leicester ndio klabu inayoongoza kumfunga Klipp(mara 3) katika ligi kuu ya nchini Uingereza kuliko timu yoyote ile.
Lakini kwa sasa barani Ulaya uwanja wa Anfield unaonekana kati ya viwanja vichungu sana kwa wapinzani ambapo hadi sasa Liverpool wameruhusu mabao 3 tu katika mechi zao 10 walizocheza Anfield.
Coutinho, Salah na Mane wanaonekana kuwa kirusi kwa wapinzani kwani ukiacha PSG na Man City, klabu ya Liverpool ndio klabu ambayo imefunga mabao mengi zaidi katika msimu huu barani Ulaya(mabao 77).

No comments:

Powered by Blogger.