Trending News>>

Chelsea vs Stoke City, Stoke wanatembelea “machinjio” yao makubwa hii leo

Michezo 9 iliyopita Stoke City wameshindwa kabisa kuwagusa Chelsea, katika alama 27 ndani ya michezo hiyo Chelsea wamechukua 25(ushindi mara 8 na suluhu 1) huku Stoke City wakichukua moja tu.
Stoke anakwenda tena katika uwanja ambao unaonekana kama machinjio yake makubwa huku hadi sasa akiwa anaongoza kwa kufungwa mabao mengi zaidi EPL, wameshafungwa mabao 41.
Chelsea ndio klabu inayoongoza kwa kuifunga Stoke City kwani katika michezo 19 waliyokutana, Stoke amekubali kufungwa mara 14 akibahatika kupata suluhu 3 na ushindi mara 2 na katika michezo yao yote 15 iliyopita wamefungwa mechi moja tu.
Chelsea hawajawahi kupoteza mchezo wao wa mwisho wa mwaka katika ligi ya EPL tangu mwaka 2011 ambapo walifungwa na Aston Villa kwa mabao 3 kwa 1, huku safari hii wakiwa wameruhusu mabao 4 tu katika mechi 11.
Ukiacha Southampton wanaocheza na Manchester United hii leo, Stoke City ndio klabu inayofuatia kwa kucheza mechi nyingi bila bila clean sheet(mechi 10) Southampton wamecheza 11 bila clean sheet.

No comments:

Powered by Blogger.