Kimenuka… Wabunge wa Tanzania, Burundi Wamkataa Spika wa EALA
SIKU moja baada ya Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika mashariki
kuchaguliwa na wajumbe wa nchi nne za jumuiya badala ya sita wabunge
kutoka Burundi na Tanzania na Burundi wamesema uchaguzi huo umekiuka
misingi na kanuni za Jumuiya hiyo.
Wakizungumza na waandishi wa habari Jijini Arusha, Mwakilishi wa
wabunge hao wamesema hakukuwa na sababu ya kutumia nguvu jazba na
uharaka wa kumchagua Spika kabla ya hoja zao ikiwemo ya kutaka kupata
ufafanuzi wa mzunguko wa kumpata spika haujatolewa na kwamba
hawakubaliani na na suala hilo na endapo hali isipodhibitiwa malengo ya
kuundwa kwa jumuiya hiyo hayatatimia.
Kwa upande wao Wabunge kutoka Tanzania wamesema hatua ya wabunge wa
bunge hilo kuanza kukiuka viapo vyao muda mfupi baada ya kuapishwa ni
dalili za kukosa moyo wa uvumilivu, umoja, na ushirikiano wa dhati ambao
kwa muda wote ndio umekuwa msingi wa jumuiya hiyo na sio dalili nzuri
hasa ikizingatiwa kuwa miongoni mwa malengo ya jumuya ni kudumisha
mshikamano na kwamba kilichofanyika ni sio kumchagua Spika bali ni maoni
yao kuwa Mh. Martin anafaa kuongoza.
Aidha Wabunge wa Tanzania wamesema kuwa wanaendelea kuziomba ngazi
zinazohusika kuangalia upya suala hilo na kutoa nafasi ya majadiliano
kwani ndio msingi wa kupata suluhu.
Kufuatia hali hiyo wabunge kutoka Burundi licha ya kudai kuwa
hawamtambui Spika aliyechaguliwa wamesema hawawezi kushiriki kikao
chochote kitakachoendeshwa na spika huyo.
Wabunge hao wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliapishwa siku ya tarehe
18 /12 /2017 na wakati wa kumchagua spika uliibuka mjadala unaodaiwa
kusababishwa na taarifa zilizotolewa na katibu wa Bunge kuwa wabunge wa
nchi zote ispokuwa uganda wanaweza kuomba kugombea uspika wakati
utaratibu wa awali ulikuwa ni wa kufuata mzunguko.
Wabunge hao wamefafanua kuwa hata kama mzunguko ungezingatiwa bado
lingehitaji ufafanuzi ambao ungezihusisha Burundi, Rwanda na Sudani
Kusini suala ambalo wanasema licha ya kuliwasilisha lilipuuzwa.
No comments:
Post a Comment