Inawezekana huyajui mambo haya 5 kuhusu Instagram
Mtandao wa Instagram ni moja kati ya
mitandao ya kijamii inayopendwa na kutumiwa na watu wengi sana duniani.
Ina watumiaji zaidi ya milioni 250 duniani kote na kumekuwa na
mabadiliko mbalimbali ambayo yamefanyika kwenye mtandao huu tangu
umeanzishwa. Vifuatavyo ni vitu 5 ambavyo yawezekana huvifahamu kuhusu
mtandao huu wa Instagram
Instagram ni nini?
Ni mtandao ambao ni kwa ajili ya kushare picha na video za matukio
yao mbalimbali. Hapo awali wakati Instagram inaanzishwa kilichofanya
mtandao huu kupenda ilikuwa ni idadi ya filter ambazo zinawezesha
mtumiaji kuhariri picha zake kwa jinsi anavyopenda. Pia Instagram ilikua
inaruhusu kupost picha za kipimo au umbo la mraba tu yaani square.
Hata hivyo mabadiliko yalifanyika ilipofika August 2015 kwenye size
za picha za kuweka kwenye mtandao huo ambapo watumiaji waliruhusiwa
kuweka picha za maumbo yoyote bila tena kulimitiwa na umbo la picha za
square.
Watu gani haswa wanatumia Instagram?
Inaelezwa kuwa mtandao wa Instagram ndio unaotumiwa na watu wa
matabaka yote ya jamii katika maeneo mbalimbali duniani. Watafiti wa
masoko wameeleza kuwa 90% ya watumiaji wote wako chini ya umri wa miaka
35 na kati yao 68% ni wanawake wakati 70% kati ya watumiaji wote duniani
hupitia akaunti zao angalau mara moja kwa siku.
Inaelezwa pia kuwa mtu maarufu duniani ambaye anapicha za selfie
nyingi kwenye akaunti yake ya Instagram ni mwanamitindo wa Marekani
Kylie Jenner ambaye ni mdogo wa Kim Kardashian ambaye ana selfies zaidi
ya 450, huku celebrity mwenye followers wengi zaidi Instagram ni
mwanamziki Selena Gomez mwenye followers milioni 128.
Instagram inatumiwa wapi?
Kwa watumiaji wa simu za mkononi, watumiaji wa Instagram ni wengi
sana kuliko wanaotumia Twitter kwenye simu zao. Japokuwa ilitengenezwa
na kuzinduliwa nchini Marekani, ni 40% tu ya watumiaji wote wa mtandao
wa Instagram wanaishi nchini humo, na nchi za Brazil na Japan ndizo
zinazoingia kwenye top 3 ya nchi zenye idadi kubwa ya wanaotumia mtandao
huo baada ya Marekani.
Instagram ilitengenezwa lini?
Mtandao huu ulitengenezwa mwaka 2010 na Kevin Systrom and Mike
Krieger. Ilizinduliwa rasmi kama programu ya Kampuni ya Apple April
2010. Na baada tu ya kuzinduliwa ilipata watumiaji milioni 1 ndani ya
mwezi mmoja na kutokana na hili, Kampuni ya Facebook iliamua kuinunua
programu hii April 2012.
Kampuni ya Facebook iliinunua App hiyo ya Instagram kwa Dola za
Marekani bilioni 1 ambayo ni sawa na takriban Tsh trilioni 2.4. Wakati
Instagram inanunuliwa na facebook, ilikua na wafanyakazi 13 tu na
ilipofika April 2012 Instagram ilianza kupatikana katika simu za Android
jambo lililoelezwa kuwa lilikuwa la mafanikio makubwa sana.
Baada tu ya Instagram kuingizwa system ya simu za Android takriban
watu milioni 1 walidownload program hii na kuanza kuitumia ndani ya
masaa 12. Ilipofika June 2013 mabadiliko kadhaa yalifanywa kwenye
mtandao huu ambapo watumiaji waliweza kuanza kupost video fupi kwenye
akaunti zao zisizozidi sekunde 15. Mabadiliko haya yalipelekea kupostiwa
video takribani milioni 5 ndani ya saa 24.
Kwanini Instagram inafahamika na kutumiwa na watu wengi zaidi duniani?
Instagram inafahamika sana kwasababu kwanza ni mtandao ambao
unapatikana bila malipo yoyote tofauti na baadhi mitandao ya kijamii
lakini pia mtandao huu umetajwa kuwa umeongeza ubunifu wa watu ambao
wanajitahidi kupost picha na video nzuri kwa kuzihariri kabla ya
kuzipost, jambo ambalo limeongeza watu kufahamiana zaidi.
Sababu nyingine ni kwamba Instagram inaruhusu watumiaji wake kupiga
na kupost picha aina ya selfie, ambazo ni picha za mtu aliyejipiga picha
mwenyewe. Inaelezwa kuwa kuna selfies zaidi ya milioni 60 zilizopostiwa
kwenye mtandao huu ambazo zina hashtag ya selfie. Inaelezwa pia kuwa
hashtag zinazotumiwa zaidi kwenye mtandao huu ni love, me, beautiful na
hashtag tbt. Na 83% ya post zote za Instagram zinaelezwa kuwa na
hashtag.
No comments:
Post a Comment