Ecobank yasaidia kupatikana kwa maji safi shule ya Hananasif
KATIKA kuadhimisha siku ya Ecobank (Desemba 9) ambayo hufanyika kila mwaka katika nchi 33 barani Afrika, Ecobank Tanzania imetoa msaada wa upatikanaji wa maji safi katika Shule ya Msingi ya Hananasif iliyopo katika Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Ecobank imeweka tanki maalumu ili kurahisisha usambazaji pamoja na upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika vyoo na maeneo mbalimbali shuleni hapo yenye uhitaji wa maji kwa wanafunzi na walimu.
Aidha benki hiyo imetoa vitabu pamoja na kukabidhi zawadi mbali mbali kwa wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la sita walioshika nafasi ya kwanza hadi ya tatuu
Akizungumza wakati wa hafla ya kufungua Kisima hicho leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mtendaji wa Ecobank, Mwanahiba Mzee amesema, msaada huo utasaidia shule hiyo kupata maji safi na salama na dhamira yao kubwa ni kuunga mkono juhudi za serikali za kuinua kiwango cha elimu nchini kwa kuboresha miundombinu.
“Tuliguswa sana baada ya kupewa taarifa kuwa shule hii inawanafunzi 728 lakini miundombinu ya maji imeziba na kubakia sehemu moja tu ambayo inatumiwa na shule nzima, vyoo havina maji na hivyo imekuwa changamoto ya kiafya kwa wanafunzi na walimu, tukaona in vyema kusaidia na kuokoa afya za watoto, amesem Mzee.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Idda Uiso amesema walikuwa wakikabiliwa na changamoto kubwa ya maji kwani kwa idadi kubwa ya wanafunzi waliopo shuleni hapo, huduma ya maji na salama ni muhimu sana.
“Kwa msaada wa maboresho ya miundombinu yaliyofanyika kwa sasa tuna uhakika wa maji safi na salama kwa walimu na wanafunzi. Vitabu pamoja na zawadi vilivyotolewa kwa wanafunzi bora, kutaongeza hamasa kwao kufanya vizuri zaidi.
No comments:
Post a Comment