Dude Aiona Krismasi Chungu
Kulwa Kikumba ‘Dude’.
Akiongea na Risasi Jumamosi ambalo lilishuhudia ajali ya staa huyo iliyotokea maeneo ya Mliman City, alisema kuwa alikuwa akitokea Arusha na wakati huo alikuwa akienda Lugalo kufuatilia gari lake ambalo alimuachia shemeji yake ndipo ajali ya pikipiki ilipomtokea.
“Unajua kilichotokea ni hivi, nilipotoka Arusha sikwenda nyumbani niliamua kufuata gari langu Lugalo ambapo nililiacha wakati nasafiri kisha ndio niende nyumbani, lakini nilipofika Mlimani tu kwenye mzunguko pale tulipata ajali nikadondoka na kuumia, lakini kilichosababisha ajali ilikuwa ni kamba iliyokuwa imefunga gari linalovutwa, kwa ajali hiyo niliiona Krismasi chungu,” alisema Dude.
No comments:
Post a Comment