Trending News>>

“Barca wanatunyanyasa wachezaji wa Brazil” De Lima amuonya Coutinho

Liverpool & Barcelona schedule Philippe Coutinho meeting to finalise £124m transfer
Phelipe Coutinho yupo njiani kutimkia La Liga, taarifa zinasema nyota huyo wa Liverpool tarehe 3 mwezi ujao anataraji kukutana na mabosi wa Barca na mambo yakienda sawa huenda akahamia huko hivi karibuni.
Lakini Ronaldo De Lima ameibuka na kumuonya nyota huyo kuwa makini kuhusu uhamisho wake wa kwenda Barcelona, De Lima amesema klabu hiyo ya Hispania huwa haikai vizuri na wachezaji toka Brazil.
Ronaldo ambaye amewahi kupita Barcelona amemtaka Coutinho kuwaza kuhusu yeye(Ronaldo), Rivaldo, Romario na Neymar jinsi walivyoondoka Barcelona na kisha ndio afanye maamuzi kuhusu kuhamia huko.
Amesisitiza kwamba mwisho wake Barcelona haukuwa mzuri hata kidogo na tangu akae Barcelona alianza kujisikia upweke huku akitamani kuhamia kwenda kucheza katika vilabu vingine.
Hivyo hivyo kwa Neymar pamoja na kuitumikia Barcelona vyema lakini kuondoka kwake haikuwa katika hali ya kuelewana na hadi sasa Neymar na Barcelona wana baadhi ya kesi kuhusu uhamisho wake.
Ronaldinho Gaucho, Rivaldo na Romario nao kwa wakati kadhaa wamekuwa na mikwaruzani na Barcelona hali inayomfanya De Lima kuwa na wasiwasi kuhusu Phellipe Coutinho.

No comments:

Powered by Blogger.