DRC: Nyumba ya Rais Kabila Yachomwa Moto
NYUMBA ya Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila imechomwa moto katika shambulizi linaloshukiwa kufanywa na waasi, ambapo askari mmoja aliuwa.
Tukio hilo limetokea Desemba 25, 2017, ambapo taarifa zinasema kuwa waasi wa kundi lijulikanalo Mai Mai walijaribu kuiba mali kutoka makazi hayo ya rais yaliyoko eneo la Musienene, katika jimbo la Kivu ya Kaskazini.
Wakati wa tukio Rais Kabila hakuwa kwenye nyumba hiyo ambayo iko kijijini maili 1,680 Mashariki mwa mji wa Kinshasa, huku kundi la Mai Mai na kundi la waasi wa ADF wakiwa washukiwa wa kwanza juu ya tukio hilo.
Hivi karibuni Rais Kabila amekuwa akipingwa na wanasiasa mbali mbali kwa kitendo chake cha kutaka kugombea nafasi ya urais kwa muhula mwengine.
No comments:
Post a Comment