Usagaji Unavyowaathiri Wasichana Tanzania-2
SUZANA anasema kuwa, alianza kushiriki vitendo vya kisagaji akiwa shule ya sekondari huko Mwanza. “Wakati nasoma huko Mwanza (anataja jina la shule), nilikuwa nikiishi bweni, kuna dada mmoja nilikuwa nalala naye na nilimchukulia dada kwa sababu alikuwa amenizidi umri.
“Kila ikifika majira ya usiku huyo dada alikuwa akiniomba nimshike na kumkumbatia, basi taratibu akaanza kunifundisha mambo hayo na baadaye nikawa mzoefu kabisa kiasi kwamba ilikuwa ni kazi ngumu mno kwangu kuacha mchezo huo,” anasema Suzana. Suzana anaendelea kusema kuwa, kwa sasa anajaribu kupambana ili aweze kuachana na vitendo hivyo maana tofauti na awali alivyokuwa msichana kamili, tangu aanze kushiriki vitendo hivyo amejikuta akipenda tabia za kiume. “Yaani hata namna ya uvaaji nilivyotoka shuleni nimebadilika kiasi kwamba wazazi wangu wakawa wananishangaa.
“Nilitokea kupenda mavazi ya kiume na kukaa na wanaume, nikawa sijiweki tena kwenye kundi la wanawake wenzangu, hali ambayo imenikosti sana maana ilifika hatua jamii nzima ikawa inanichukulia tofauti hata wazazi wangu pia hawakufurahishwa na mimi. “Umefika umri nataka kuolewa imekuwa tabu kweli, najikuta nikikosa hata mchumba.”
Mwanadada mwingine aitwaye Malkiz ambaye aliwahi kukiri hadharani kwamba ni msagaji na ameshafanya hivyo kwa wadada wengi wakiwemo wake za watu na michezo hiyo alianza akiwa mdogo wakati anasoma shule ya bweni, ndipo akanogewa na kuendelea hadi ukubwani huku akikiri kutovutiwa kabisa na wanaume.
“Ni kweli haya mambo yamezidi kushika kasi, lakini kitu kinachopelekea haya ni kutokana na tamaa, utandawazi na vishawishi,kwa maana kwamba mtu anayefanya mambo haya anaweza akavutiwa na mdada mrembo ambaye hajui kabisa michezo hiyo, lakini akamshawishi kwa kigezo cha pesa naye akakubali.
“Kuna wadada wazuri tu ambao wanafanya hii michezo licha ya kwamba wana mabwana zao na wanawapa huduma nzuri wanapokuwa faragha lakini wanaharibiwa na hizi filamu chafu za Kizungu ambapo wakiziangalia kwa jinsi wanavyosagana basi hujikuta wakitamani taratibu na mwisho wa siku wanadumbukia huko,” anasema Malkiz.
Mbali na Malkiz, Ijumaa limefanikiwa kuzungumza na wadada wengine wawili ambao hawakuwa tayari majina yao yaanikwe gazetini. Kimaumbile wadada hawa wameumbika kiasi cha kumtamanisha mwanaume mwenye uchu lakini wasichokijua wengi ni kwamba wanajihusisha na usagaji licha ya kuwa na wapenzi wao wa kiume. “Niwe mkweli tu mimi nasagana lakini nakuwa na wanaume kama kawaida, kitu kinachonipelekea hivyo ni stress za mapenzi.
Unakutakila mwanaume unayekuwa naye kwenye uhusiano ni maumivu tu, mtu unampenda unaamua kutulia naye lakini mwenzako michepuko haikauki au anakudharau heshima ya penzi lenu haipo basi inabidi uingie upande wa pili kwa hiyo huku upo kawaida lakini upande mwingine unajipoza,”anasema mmojawapo. Kwa upande wa mwanadada mwingine anasema, jambo ambalo lilimuathiri na kujikuta anaingia kwenye vitendo vya kusagana ni kutokana na tabia aliyokuwa ameiendekeza ya kupenda kuangalia filamu za ngono kwa maana ya jinsi mbili tofauti.
“Nilikuwa nikipenda sana kuangalia filamu za ngono hasa za Kizungu kila nikitaka kulala lakini nilikuwa naangalia za jinsia mbili tofauti, sasa baada ya kuzizoea, ndipo nikaona ngoja nigeukie kutazama na filamu za usagaji kwa kuwa nilikuwa nikisikia kwa watu wanasifia kusagana hakuna stress kama kuwa na mwanaume. “Baada ya kuangalia kwa muda nikawa najaribu kujihudumia mwenyewe kutokana na hamasa ninayoipata kwenye hizo filamu hadi nikazoea. Nadhani tabia ya mwanamke kutaka kukidhi haja zako mwenyewe pia inachangia sana kuingia kwenye usagaji, sababu raha unayoihisi unaona kumbe hata mwanamke mwenzio akikufanyia hivyo utaridhika siyo lazima mwanaume.
“Siku moja sasa nikawa nimeenda saluni ya kike, kuna wadada wanapiga stori za kusagana wakisifia mchezo huo, nikawa nahoji raha zake ndipo mmoja wapo akaanza kunishawishi tukajaribu nijionee mwenyewe, nikakubali kwa kuwa zile filamu tayari zilikuwa zimeshanitamanisha na kujaribu kwa mdoli, tangu hapo nikanogewa huu ni mwaka wa tatu sijawahi kuacha japo nakuwa na wapenzi wa kiume pia.” Mdada huyo anaendelea kusema kuwa, kinachopelekea japo wanakuwa wanasagana lakini wanaendelea kuwa na wanaume, ni kwa sababu kusagana ni starehe tu ya kuwapa amani ya moyo licha ya kuwa wanakuwa na hisia na wivu kwa mtu wanayemzimikia, pia wanakuwa na hisia na wanaume vilevile ndiyo maana mtu wa hivyo anaweza
kufanya vyote kwa pamoja.
Viongozi wa dini wanasemaje? Kwa upande wa Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum anasema kuwa ushoga na usagaji ni moja ya matokeo ya mmonyoko wa maadili, watu wanapoacha kufuata sheria na taratibu za Kimungu matokeo yake ni kuibuka kwa matukio ya namna hii. “Kwa mujibu wa mafundisho ya dini ya Kiislamu inapobainika umefanya kosa la kuingiliana kimwili kati ya mwanaume na mwanaume ama kati ya mwanamke na mwanamke mwenzake hukumu ya watu wa namna ni kukatwa kichwa.
“Mantiki ya hukumu hii ni kuwaponya mamilioni ya watu wengine ambao walikuwa na mpango wa kutenda kosa hilo, vijana hawana budi kuoa na kuwatumia wake zao kwa mahitaji ya miili yao hata pia kwa wanawake kuolewa.” Aidha, Alhad ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa uthubutu wake wa kuchukua hatua katika kupambana na vitendo mbalimbali vya kihalifu ikiwa ni pamoja na kukomesha vitendo vya kishoga na usagaji sanjari na dawa za kulevya.
“Pongezi zangu kwa Serikali ya Awamu ya Tano, iendelee na juhudi ya kupambana na watu wenye tabia za namna hii kwa kutunga sheria kali zaidi ili kukomesha tabia hizi chafu mathalani matukio ambayo yamekuwa yakitokea nchini ambayo yamekuwa yakifanywa na watu wenye tabia za kishoga ni zile sherehe za kila mwaka ambazo huwa zinafanyika huko Zanzibar maarufu kama usiku wa HoneyMoon. “Kadhalika utalii umekuwa ni moja ya chanzo kikubwa cha mmomonyoko wa maadili kwa watoto wetu,” alisema Alhadi. Itaendelea wiki ijayo…
No comments:
Post a Comment