Tajiri Salaah Amkana Uwoya
DAR ES SALAAM: Tajiri mmoja maarufu jijini Dar, anayefahamika zaidi
kwa jina moja la Salaah, amemkana muigizaji Irene Uwoya ambaye amekuwa
akijinasibu kwenye mitandao ya kijamii kuwa ni mpenzi wake.
Kumekuwa na habari zinazozagaa mitaani kuwa Uwoya, mke wa zamani wa
mwanasoka Hamad Ndikumana, ndiye anayekula maisha na mfanyabiashara huyo
na kuthibitisha hivyo, muigizaji huyo ambaye yupo levo ya daraja la juu
(A List Female Artist) siku chache zilizopita alionekana katika kipande
cha video katika mtandao mmoja akiwa amejichora tattoo yenye jina la
mvulana huyo.
“Habari kubwa mjini ni kuhusu Uwoya, inasemekana jamaa amekufa ameoza
kwa shostito na mwanamke jinsi anavyojua kuweka sawa mambo kachora hadi
tattoo mgongoni mwake yenye jina lake,” kilisema chanzo chetu ambacho
ni miongoni mwa wasiri wa muigizaji huyo.
Risasi lilijaribu mara kadhaa kumfikia kwa njia ya simu Uwoya bila
mafanikio, kwani mara zote simu yake iliita bila kupokelewa na hata
alipotumiwa ujumbe mfupi wa simu, hakujibu lolote. Salaah ambaye
anadaiwa kuwa kijana mwenye fedha na anayefahamika sana miongoni mwa
mastaa kutokana na ukwasi mkubwa alionao, alizungumza na Risasi
Mchanganyiko akiwa nje ya nchi na kudai hajui chochote kinachozungumza
juu yake na msichana huyo. “Sikiliza, mimi hayo mambo unayozungumza
siyajui na wala huyo unayemtaja simjui, ndiyo kwanza nakusikia wewe,
tafadhali usinihusishe na hayo mambo mimi siyajui,” alisema kwa kifupi.
No comments:
Post a Comment